In Summary
  • Kwenye post hiyo aliwaambia mashabiki wake kuwa wanatakiwa kutafuta pesa hadi ex wao awapigie simu na kuwasihi waambie umma kuwa walikuwawakichumbiana siku za nyuma
Mfanyabiashara Jimal Rohosafi
Image: Instagram//JimalRohosafi

Mfanyabiashara, Jamal Rohosafi amekosolewa vikali na wanamitandao kufuatia chapisho lake la hivi punde la mafumbo kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, kwenye chapisho hilo, alikuwa akiwakejeli  wapenzi wake wa zamani.

Kwenye post hiyo aliwaambia mashabiki wake kuwa wanatakiwa kutafuta pesa hadi ex wao awapigie simu na kuwasihi waambie umma kuwa walikuwawakichumbiana siku za nyuma,

Ujumbe ambao ulivutia hisia za watumiaji wengi wa mtandao huku wengi wakisema anamzungumzia Amber Ray na Amira.

"Pata pesa hadi mpenzi wako wa zamani akupigie simu na kukuambia "Naomba uwaambie marafiki zangu kuwa tulichumbiana kwa maana hawaniamini,"✌️

Wachache walitoa maoni chanya huku wengi wakitoa maoni yasiyofaa, waliotoa maoni ya udhalili walikuwa wakimdhihaki Jamal wakidai kwamba anasema uongo kuhusu mwanasosholaiti Amber Ray na Amira

Wale ambao alitoa maoni chanya walikuwa wakimshukuru kwa msukumo na motisha ya kufanya kazi kwa bidii.

Hizi hapa baadhi ya hisia zao;

official_mlocc: Vile amberay anasema sai😂

_sharo.nmiles:Some old and idle women be commenting with hatred na akuna kitu wakonayo💔 just learn to appreciate people..

wildaan66: Mambo na ex tumekuachia wwe😎.....tafuta mwanamke legit banaa

winnilisakabuu: Amber ndio alikua anafanya ukae vizuri aki 😏... Kama ni weightloss journey tupewe tips baaassss

mwachiamadeda:  Sasa kuja mbololo tukupee bibi mali safi uwache kuteseka na kutesa madem wawatu bure😂😂😂😂😂 unahitaji kienyeji yenye imechemka vizuri

jane_body_massage_scrubbing: Don't you know once a lady is done she mean it?Especially our Amira...utajua hujui na pesa zako

View Comments