In Summary
  • Kuwa familia yenye maombi, kwao, ilikuwa ni ufunuo kwamba Mungu daima huwaangalia

Familia ya Wajesus, Kabi Wajesus almaarufu Peter Kabi na Millicent Wambui almaarufu Milly Wajesus leo wamefichua ni kwa nini walimfukuza yaya wao.

Wakizungumza kwenye chaneli yao ya YouTube iliyopewa jina la "Wajesus Family" walifichua kuwa wayaya wao wawili walikuwa wamesafiri kwa msimu wa sikukuu hivyo ilibidi wamtafute yaya mwingine.

Hatimaye walipata mmoja kutoka Uganda kupitia kwa rafiki wa karibu lakini Milly alihisi kitu cha ajabu kuhusu utu wa yaya. Yule yaya alikuwa akizembea jambo ambalo lilimfanya Milly kupekua begi la yaya.

Walikutana na kitu ambacho Milly alidhani ni uchawi tu kugundua kuwa ni bhangi.

"Msichana ameleta bangi nyumbani kwetu kutoka Uganda. Hiki ndicho kitu cha kichaa zaidi ambacho tumewahi kuona." Kabi

Milly alikasirika na akaapa kwamba hatamwamini mtu yeyote na watoto wake tena.

"Jamani nimechanganyikiwa. Ninajisikia vibaya sana. Sijui kama nitawahi kumwamini mtu yeyote na watoto wangu. Yaya yeyote, namshukuru Mungu kwa roho mtakatifu ameniguide ni asilimia mia roho mtakatifu nataka nimuachie tu aende ama tufike mahali alale na asubuhi anaondoka siwezi kumudu hii." Milly Alizungumza.

Kuwa familia yenye maombi, kwao, ilikuwa ni ufunuo kwamba Mungu daima huwaangalia.

"Hii ni ishara tu kwamba Mungu bado anatuangalia. Anailinda nyumba yetu, anailinda familia yetu, analinda watoto wetu." Kabi

 

 

 

 

View Comments