In Summary

•Rayvanny alichapisha  video inayomuonyesha akimsindikiza mama huyo wa mtoto mmoja hadi uwanja wa ndege na kumuaga.

•Haya yanajiri wiki moja tu baada ya wawili hao kuthibitisha wamerudiana, takriban miaka mitatu baada ya kutengana.

Rayvanny na Fahyma katika uwanja wa ndege.
Image: INSTAGRAM// RAYVANNY

Staa wa Bongo Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny ameendelea kudhihirisha mahaba yake mazito kwa mzazi mwenzake, Fahymah.

Siku ya Jumapili, bosi huyo wa Next Level Music alikiri jinsi anavyom'miss mpenzi huyo wake baada ya kusafiri kuenda mbali naye.

Rayvanny alichapisha  video inayomuonyesha akimsindikiza mama huyo wa mtoto mmoja hadi uwanja wa ndege na kumuaga.

"Nimekumiss, si urudi basi @fayvanny," aliandika chini ya video hiyo,

Hata hivyo, hakufichua maelezo ya safari ya mpenzi huyo wake  hivyo alikoelekea na alichoenda kufanya bado ni kitendawili.

Haya yanajiri takriban wiki moja tu baada ya wawili hao kuthibitisha wamerudiana, takriban miaka mitatu baada ya kutengana.

Wawili hao walithibisha kufufuka kwa mahusiano yao yaliyosambaratika takriban miaka mitatu iliyopita, siku chache zilizopita baada ya Rayvanny kumshirikisha mpenziwe huyo katika video ya wimbo wake mpya 'Forever.'

“Mtoto mbichi teketeke aki Mama umelainika. Umeumbika, acha nikumwagie sifa. Waruke sakara na mateke uzuri wako hawatofika, mama umejazisha, mikate ya kumiminisha,” Rayvanny alimsfia Fahyma kwenye wimbo huo.

Siku chache baada ya kuachia wimbo huo, bosi huyo wa Next Level Music alithibitisha hata wanaishi pamoja baada ya kurudiana.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, alichapisha video yake na Fahyma wakiwa wametulia pamoja kitandani.

"Amka, amka.. Hongera, umetimiza milioni moja kwa siku moja," Rayvanny alisikika akimwambia mpenziwe siku ya Jumatatu.

Baadaye, Rayvanny alifichua kuwa kufanya mazoezi ni mojawapo ya masharti aliyowekewa na mzazi mwenzake baada ya kurudiana

"Haya ni masharti mapya ya shemeji yenu. Lazima nifanye mazoezi kila siku. Mimi nitakufa. Tuende," msanii huyo wa zamani wa WCB alisema kwenye video iliyomuonyesha akifanya mazoezi ya nje peke yake.

Rayvanny na Fahymah walitengana mwaka wa 2019 ambapo kila mmoja aliamua kuenda njia yake. Baada ya kutengana, haikumchukua Rayvanny muda  mrefu kabla ya kuzama kwenye huba zito na bintiye Kajala, Paula Paul.

Hata hivyo, mwaka jana, bosi huyo wa Next Level Music alidokeza kuvunjika kwa mahusiano yake na mwanamitindo huyo wakati akitumbuiza katika tamasha la Fiesta 2022 mjini Sumbawanga, Tanzania.

"Mapenzi yasikuchanganye nakwambia, usije ukapata bila kama Dulla. Mapenzi usije kufananisha,  kama  vile chakula. Nilinyosha moyo Karula, nikaachana na Paula..." aliimba

View Comments