In Summary

"•"Naona wanarika wa mama yangu (miaka 35) wana watoto wadogo wengine hawana mtoto hata mmoja na mama yangu ana mimi." alisema.

•Mwaka wa 2022, Purity aka Pritty alifichua maisha ya familia yake akifichua kuwa mama yake alitatizika kumlea.

Pritty Vish Mwanablogu asherehekea siku yake ya kuzaliwa
Image: Facebook

Mwanasholaiti mzaliwa wa Kibera, Pritty Vishy amefichua kuwa mamake alikuwa mzazi akiwa na umri mdogo wa miaka 14.

Mwanasholaiti huyo alikuwa akizungumza kuhusu umri wa uzazi.

"Naona wanarika wa mama yangu (miaka 35) wana watoto wadogo wengine hawana mtoto hata mmoja na mama yangu ana mimi."

Vishy anaona umri ambao mamake alimpta kama mdogo lakini anamlinganisha na wengine.

"Yaani msichana mzima mzima ananifanya nijisikie kuzidiwa na hisia. Nafikiria alinibeba tumboni mwake kwa muda wa miezi tisa akiwa na miaka 14 wakati mwingine nilimtazama na kushindwa kufikiria jinsi alivyojitahidi kunibeba."

Mwaka wa 2022, Purity aka Pritty alifichua maisha ya familia yake akifichua kuwa mama yake alitatizika kumlea.

Alisema kuwa alilelewa na mama pekee yake. Mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 21 alikiri kwamba akiwa mama single, mamake alijaribu kila njia ili kujikimu, na hivyo ndivyo alivyoingia katika maisha ya makanga.

Pritty pia alifichua kuwa uhusiano wake na babake ulikuwa umesambaratika tangu alipomtelekeza akiwa mdogo na haoni haja ya kufanya mambo yaende.

"Uwepo wako kama mzazi ni muhimu na ndio huko usoni ukipata kidogo unawapea juu ni wazazi kwa sababu walikuwepo kwa ajili yako. 

Nilikuwa nikienda kwa baba yangu mzazi nikimwambia nahitaji nguo za Krismasi mwaka wa 2019, lakini aliniambia hana pesa na kitu kizuri nilipata ndani ya nyumba yake wakati alikuwa amenunua nguo za watoto wake wa kambo."

Mama yake aliolewa tena, lakini hatimaye walitengana na baba yake wa kambo, na mama yake alihitaji kujikimu.

"Ilibidi ameingia makanga kwa sababu alienda shule ya udereva na akakua makanga juu si rahisi lazima ukue na driving license. So kukua makanga ilikua inamlipa vizuri juu labda siku moja anagelipwa 2k kukiwa na kubaya kabisa 1k or 700 hivyo so akafanya fanya."

Vishy pia aliambia Mpasho katika mahojiano Aprili 2022 kwamba mama yake amefanya kazi kama mfanyakazi wa ndani nchini Saudi Arabia tangu 2019.

View Comments