In Summary

•Arap anatumai kukamilisha safari hiyo ngumu ambayo imemchukua siku kadhaa hivi leo, Jumanne anapotarajia kuwasili Nairobi.

•Arap alieleza ombi lake kwamba waziri wa michezo Ababu Namwamba awe katika Barabara ya Bunge kumkaribisha anapowasili.

Arap Uria amejawa bashasha baada ya Drury kumtakia heri akiendesha baiskeli kutoka Eldoret hadi Nairobi
Image: FACEBOOK// ARAP URIA

Wiki iliyopita, mchekeshaji Arap Uria alianza safari kutoka Eldoret hadi Nairobi kwa baiskeli katika hatua ya kutimiza ahadi aliyokuwa ametoa.

Shabiki huyo wa klabu ya soka ya Chelsea diehard iiapa kuendesha baiskeli kwa safari hiyo ya zaidi ya kilomita 300 iwapo timu hiyo aiipendayo ingeshindwa na Manchester United katika mchuano wao mkubwa wa Mei 25.  Ndani ya dakika 90 za mechi hiyo, The Blues walipokea kichapo cha  4-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.

Arap anatumai kukamilisha safari hiyo ngumu ambayo imemchukua siku kadhaa hivi leo, Jumanne anapotarajia kuwasili Nairobi.

"Safari imezidi kuwa ngumu lakini nitaikamilisha kesho. Mwisho ni kwenye Barabara ya Bunge," alisema siku ya Jumatatu.

Kulingana na taarifa zake za moja kwa moja, mchekeshaji huyo alivuka hadi kaunti ya Kiambu Jumatatu na akasimama Limuru.

Pia alionyesha ujumbe mzuri kutoka kwa mtangazaji maarufu wa soka Peter Drury ambaye alimtakia heri katika safari yake.

"Habari Arap, ni Peter hapa, nakutakia kila la kheri kwenye safari yako kubwa ya kuelekea Nairobi. Uwe salama, furahia na ninatazamia kuzungumza nawe tena," Drury alisema kwenye video ambayo Arap alishiriki kwenye Facebook.

Arap aliyeonekana kufurahishwa sana na ujumbe wa Drury aliusherehekea na kumshukuru kwa maneno yake mazuri.

"Tunahitaji marafiki kama hawa maishani. Asante sana Peter Drury. Mwisho ni kesho katika Barabara ya Bunge saa sita adhuhuri," Arap alisema Jumatatu.

Mchekeshaji huyo pia alieleza ombi lake kwamba waziri wa michezo Ababu Namwamba awe katika Barabara ya Bunge kumkaribisha anapowasili jijini Nairobi Jumanne. Tunamtakia Arap kila la heri anapoendelea na safari yake.

View Comments