In Summary

•Benki ya Stanbic na Radio Africa Events zimewaahidi wateja na mashabiki burudani ya kukata na shoka na ya kukumbuka daima.

•Bendi ya nyumbani ya Sauti Sol iliyoshinda tuzo nyingi itakuwa sehemu ya wasanii waliopangwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Tiketi zate za Stanbic Yetu Festival zimeuzwa
Image: RADIO AFRICA EVENTS

Huku zikiwa zimesalia siku 7 pekee kwa Tamasha la Stanbic Yetu lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na ghamu kufanyika, tikiti zote zimeisha!

Benki ya Stanbic na Radio Africa Events zimewaahidi wateja na mashabiki burudani ya kukata na shoka na ya kukumbuka daima.

Tamasha hilo linaambatana na matarajio ya waandalizi kuwapa Wakenya tajriba ya kipekee, isiyosahaulika na ya kweli ya muziki wa moja kwa moja ambayo itaacha kumbukumbu ya kudumu.

Pia ni sehemu ya urithi wa kudumu wa Stanbic ya kusaidia na kukuza talanta ndani na nje ya nchi.

Tamasha la mwaka huu linatazamiwa kuwa bora zaidi ikilinganishwa na matamasha ambayo yalilofanyika miaka iliyotangulia huku likiratibiwa kuleta nchini bendi ya Boyz II Men - mojawapo ya makundi ya R&B mashuhuri katika historia ya tasnia ya muziki.

Wale ambao wamekuwepo kwa "muda" watakuambia kuwa kikundi hicho kimefafanua upya muziki maarufu na kinaendelea kutengeneza nyimbo maarufu ambazo zinavutia mashabiki katika vizazi vyote baada ya kuandika na kucheza nyimbo za zamani zilizosherehekewa na zinazojulikana zaidi kwa miongo miwili iliyopita.

Bendi ya nyumbani ya Sauti Sol iliyoshinda tuzo nyingi itakuwa sehemu ya wasanii waliopangwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Bendi hiyo itaburudisha mashabiki kwa safu ya muziki kutoka kwa albamu zao 5 na EP 1, ambazo zilipokelewa vyema nchini na duniani kote.

Zaidi ya hayo, ma-DJ mashuhuri kama vile DJ Shaky, G-Money, DJ Grauchi, DJ Dream, CNG, na DJ Forest watakuwepo ili kutumbuiza kwa michanganyiko ya nyimbo ambazo zitasimuliwa kwa vizazi vijavyo kupitia vitabu na hadithi za watu.

Tamasha hilo limepangwa kufanyika Juni 10, 2023, katika Uhuru Gardens.

View Comments