In Summary

•Tembu Daniel alianza safari ya kulia kwa saa mia moja bila kukoma mapema wiki hii akiwa na matumaini ya kuweka rekodi mpya ya dunia.

•Mashabiki wameendelea kumtia moyo kwenye ubia wake hata wengine wakionekana kukejeli rekodi anayokusudia kuivunja.

Image: INSTAGRAM// TOWNCRYER

Mwanaume mmoja kutoka nchi ya  Cameroon, Afrika Magharibi yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya muda mrefu zaidi mtu binafsi akilia bila kukoma.

Tembu Daniel, almaarufu Town Cryer alianza safari ya kulia kwa saa mia moja bila kukoma mapema wiki hii akiwa na matumaini ya kuweka rekodi mpya ya dunia.

Kwa idhini ya Rekodi za Dunia za Guinness, kama ilivyothibitishwa katika bango ambalo alshiriki, Daniel anadhamiria kufikia mafanikio hayo ya kushangaza.

“Nitaenda kuvunja rekodi ya dunia ya Guiness kwa muda mrefu zaidi nikilia. Nahitaji usaidizi wenu,” Daniel alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumapili.

Baadaye alishiriki klipu ya video iliyoonyesha akianza safari yake ya saa 100 za kilio ambapo alionekana akiwa ameketi kwenye kiti huku saa kubwa iliyokuwa ikisonga ikiwa kando yake.

Katika taarifa nyingine, mtayarishaji wa maudhui huyo ambaye kwa sasa anaishi Lagos, Nigeria alionyesha kuwa tayari alikuwa amelia kwa masaa mawili. Pia aliwataarifu wafuasi wa mtandaoni baada ya kulia kwa zaidi ya saa tano.

Mashabiki wameendelea kumtia moyo kwenye ubia wake hata wengine wakionekana kukejeli rekodi anayokusudia kuivunja.

Tazama baadhi ya jumbe za wanamitandao:

hunta.man Je tunaweza kumpatia matatizo yetu ili alie kwa ajili yetu.

melany_winter Kufikia wakati unamaliza kulia, utakuwa umeunda mto wako mwenyewe.

_tochukwu Bro, naomba kama unahitaji mambo zaidi ya kufanya ulie, tafadhali nitafute. Nina hadithi nyingi za kusikitisha za kukuambia.

kur_rency Tuko nyuma yako kaka endelea, ikiwa Guiness hawatasikia kilio chako, Mungu atasikia.

black_dollar_chief Wanigeria pia wanapenda njia ya mkato ya ukuu.

View Comments