logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchekeshaji Eric Omondi afichua lengo kuu la kudai milioni 50 ili kufichua uso wa binti yake

Mchekeshaji huyo alisema kwamba hiyo ni njia tu ya kuchanga pesa ili aweze kuwasaidia watu.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani02 August 2023 - 09:26

Muhtasari


  • •Eric amefunguka kuhusu jinsi anapanga kutumia pesa anazolipisha ili kufichua sura ya mtoto wake ambaye bado hajazaliwa.
  • •Mchekeshaji huyo alisema kwamba hiyo ni njia tu ya kuchanga pesa ili aweze kuwasaidia watu.
akizungumza nje ya KICC mnamo Agosti 1, 2023.

Mchekeshaji maarufu Eric Omondi amefunguka kuhusu jinsi anapanga kutumia mamilioni ya pesa anazolipisha ili kufichua sura ya mtoto wake ambaye bado hajazaliwa.

Wiki iliyopita, mchekeshaji huyo ambaye taaluma yake imegubikwa na utata mwingi alitangaza kuwa anahitaji kulipwa shilingi milioni 50 ili kufichua sura ya bintiye wakati akizaliwa.

“Kuona sura ya mtoto wangu itakuwa ni pesa nyingi sana, ili niifichue sura ya mtoto wangu nipewe shilingi milioni 50. Atakayenipa hizo pesa hata iwe gazeti utaziona hapo. Uso wa mtoto wangu ni mgumu sana kuona,” Eric alisema.

Aliongeza, “Namlipa kiasi hicho kwa sababu ni mtoto wa kipekee, usisahau ni ya Eric Omondi, na kwa kigezo hicho pekee ni milioni 50. Ni mrembo sana, nilimuona jana kwa scan. Tayari wakati anachunguzwa, naweza kumuona akitabasamu tu."

Katika mahojiano ya kipekee na Radio Jambo, Eric aliweka wazi kuwa halipishi kufichua uso wa mwanawe kwa manufaa yake binafsi bali anafanya hivyo kwa ajili ya Wakenya wanaoteseka katika nyakati hizi ngumu za kiuchumi.

Alisema kuwa hiyo ni njia tu ya kuchanga pesa ili aweze kuwasaidia watu.

"Ninachanga pesa kusaidia watu. Ndio, kuona uso wa mtoto wangu, unatoa 50k namsaidia kijana. Saa hii ni ujanja tu, lazima tusurvive. Ni kubaya," Eric alisema.

Mchekeshaji huyo alikuwa amejitokeza nje ya ukumbi wa KICC siku ya Jumanne mchana ili kuonyesha sapoti yake kwa maelfu ya Wakenya waliokuwa wamekusanyika hapo kujiandikisha kwa sarafu tata ya World Coin.

Akizungumzia kuhusu sarafu hiyo ya kidijitali yenye utata ambayo tayari imesimamishwa na serikali, mchekeshaji huyo alisema kuwa Wakenya wako tayari kufanya lolote ili tu kupata pesa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.

“Hatujali, tumekata tamaa sana, ukitaka nijiunge na ibada ya shetani, niuze figo zangu, hakuna kazi kwangu ni kazi hatari lakini ni lazima watoto wetu wale. Tukiuza utambulisho wetu, tukiuza roho zetu, tayari serikali imetuvuruga, nataka mtoto apata chakula tu,” alisema.

Eric alimwomba rais William Ruto afanye kazi ili kuboresha uchumi na pia kubuni nafasi za kazi kwa mamilioni ya vijana wa Kenya ambao wanatatizika kwa sasa kutokana na ukosefu wa pesa mifukoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved