In Summary

•Karen Nyamu alichapisha picha yake na Samidoh iliyopigwa jijini Dubai takriban miaka mitatu iliyopita na kusimulia masaibu yaliyompata katika kipindi hicho baada ya simu yake kupotea.

•Mwezi uliopita, Karen Nyamu alifichua kwamba amekuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki Samidoh kwa takriban miaka mitano.

Samidoh na Karen Nyamu
Image: FACEBOOK// KAREN NYAMU

Siku ya Alhamisi, Agosti 3, seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu alishare kumbukumbu yake maalum na mpenzi wake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Mwanasiasa huyo mtata alichapisha picha yake na Samidoh iliyopigwa jijini Dubai takriban miaka mitatu iliyopita na kusimulia masaibu yaliyompata katika kipindi hicho baada ya simu yake kupotea.

Nyamu pia hakukosa kukejeli jinsi baba huyo wa watoto wake wawili wadogo alivyomshika kwenye picha hiyo.

"TBT mwaka ni 2020 huko Dubai. Wadau hapa ni kama nilikuwa nimepigwa ngeta ama. Na kuna simu yangu mpaka wa leo sijawahi kupata, ilipotea hii siku. Mtupe ni msanye,” Karen Nyamu aliandika chini ya picha hiyo.

Katika picha hiyo, wapenzi hao wawili ambao uhusiano wao umejaa drama tele walionekana kuwa na furaha na nyuso zao zilifunikwa na tabasamu kubwa.

Chini ya chapisho, Samidoh alijibu, “Ningejishuku lakini techno?? (Kwa sauti ya Nyako.”

Penzi la seneta Karen Nyamu na Samidoh limeonekana kunoga na kuwa hadharani zaidi katika siku za hivi majuzi hasa baada ya mke wa kwanza wa mwimbaji huyo wa Mugithi, Edday Nderitu kuhamia Marekani takriban miezi miwili iliyopita.

Mwezi uliopita, Karen Nyamu alifichua kwamba amekuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki Samidoh kwa takriban miaka mitano.

Katika mahojiano na  Ala C kwenye kipindi cha Reke Ciume na Ene, seneta huyo wa UDA alifichua kwamba alikutana na baba huyo wa watoto wake wawili wadogo katika shughuli za kisiasa.

Hata hivyo, alikanusha madai uwa waliunganishwa na Mike Sonko kama alivyodai gavana huyo wa zamani wa Nairobi katika siku za nyuma. 

"Sonko alidhani hivyo (alikuwa ametuunganisha), lakini hata wakati ule tukiwa Dubai tulikuwa tunajuana. Sonko alikuwa bosi wangu, nililazimika kumficha white. Nilikuwa nimeficha white kwa hiyo alidhani yeye ndiye aliyefanya hivyo, kumbe tulikuwa tumezungumza (na Samidoh)," Nyamu alisema.

Seneta huyo pia alikanusha madai ya kuvunja ndoa ya Samidoh na ya 'kumuiba' mwimbaji huyo wa Mugithi kutoka kwa mkewe wa miaka mingi, Edday Nderitu.

“Sijawahi kumuibia mtu mume, tena huyo mwanaume, nina watoto naye na anapenda watoto. Ukitaka kugombana na kutofautiana naye, jaribu kumtenga na watoto wake, wote,” alisema.

Nyamu alidokeza kuwa mzazi mwenzake ameweza kutunza nyumba zake zote mbili, yake na ya Edday Nderitu kwa miaka mingi.

Aidha, alidokeza kwamba licha ya drama zote katika maisha yake ya mahusiano, yeye ni mwanamke mwaminifu sana na huwa anampigania tu Samidoh kwa sababu ni baba wa watoto wake.

View Comments