In Summary

•Raburu ambaye alitambulishwa na TV47 siku ya Jumanne alisema kwamba atakuwa anaongoza kipindi cha Wabebe Xperience kila Ijumaa.

Willis Raburu katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Mwanahabari Willis Raburu amepata makao mapya baada ya kuondoka Citizen TV.

Raburu ambaye alitambulishwa na TV47 siku ya Jumanne alisema kwamba atakuwa anaongoza kipindi cha Wabebe Xperience kila Ijumaa.

“Welcome to the new journey… THE WAIT IS OVER! Announcing my partnership with TV 47 Kenya! WABEBE! #WabebeXP” mtangazaji huyo aliandika kwenye mtandao wa facebook.

Punde tu baada ya kuondoka Citizen TV Raburi alikuwa amedokeza kwamba huenda angeendelea kunoa makali yake katika nyanja ya mziki.

View Comments