In Summary

•King Kaka alibainisha kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 sasa yuko tayari kuandika kitabu kuhusu safari yake ya soka.

•King Kaka alimshauri Olunga jinsi atasimulia alivyozaliwa na kulelewa katika vitongoji duni hadi kufikia mafanikio mengi katika soka.

King Kaka amemshauri Nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga kuandika kitabu kufuatia hatua yake kubwa aliyoifanya Jumanne usiku.
Image: INSTAGRAM

Rapa wa Kenya Kennedy Ombima almaarufu King Kaka amemshauri nahodha wa Harambee Stars Michael Olunga kuandika kitabu cha maisha yake kufuatia hatua yake kubwa aliyopiga siku ya Jumanne usiku.

Siku ya Jumanne, mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Al Duhail nchini Qatar alicheza kwenye uwanja mmoja na mshambulizi mahiri wa Portugal, Christiano Ronaldo na hata kufunga bao dhidi ya klabu yake ya Al Nassr.

Licha ya Al Duhail kushindwa 4-3 na Klabu hiyo ya Saudi Arabia, Olunga alisherehekea kwa fahari baada ya kufanikiwa kufunga bao moja na kupeana assist katika mechi ya Ligi ya Mabingwa ya Asia iliyochezwa katika Uwanja wa Al-Awwal mjini Ritadh, Saudi Arabia.

"Pambano la moyo dhidi ya mpinzani mzuri. Chagua mazuri. Naangazia mechi ya mkondo wa pili @DuhailSC. Bao na Assist,” Olunga aliandika kwenye mtandao wa kijamii.

Mashabiki wengi wa kandanda kwenye mitandao ya kijamii wameendelea kumpongeza nahodha huyo wa Harambee Stars kwa mafanikio yake makubwa na kumtia moyo kuendelea zaidi.

Katika ujumbe wake za pongezi, rapa King Kaka alibainisha kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 sasa yuko tayari kuandika kitabu kuhusu safari yake ya soka. Hata alienda mbali zaidi kumpa mawazo ya jinsi sura ya kwanza ya kitabu hicho inavyopaswa kuwa.

“Mfalme!! Sasa uko tayari kuandika kitabu na mstari wa kwanza unapaswa kuwa, "Nilifunga usiku ule na nilipokuwa nikisherehekea, niliona masikitiko kwenye uso wa mshindi wa mara tano wa Ballon D' Or Christiano Ronaldo," King Kaka aliandika chini ya chapisho la Olunga la Instagram.

Mwanamuziki huyo alimshauri Olunga jinsi katika kitabu chake atasimulia kisa cha jinsi alivyozaliwa na kulelewa katika vitongoji duni hadi kufikia mafanikio mengi katika soka.

"Ndio nilikuwa katika picha moja, uwanja mmoja na bingwa wa dunia lakini hadithi yangu haikuanzia hapo, wacha niwarudishe kwenye ghetto za Lucky Summer, mbingu ndogo ya mabanda nchini Kenya." aliandika.

King Kaka alikamilisha ujumbe wake kwa nahodha wa Harambee Stars kwa kueleza heshima yake kwake kufuatia ufanisi wake.

View Comments