In Summary

•Diana alifichua kuwa mwanawe alipata noti za pesa zilizowekwa kwenye maua kama zawadi ya nne, jambo ambalo lilimfurahisha sana.

•Morgan alimshukuru mwimbaji Bahati kwa kumtunza na kubainisha kuwa hangeweza kufika hatua aliyofikia kama si yeye.

Morgan alizidiwa na hisia baada ya Bahati na Diana Marua kumsherehekea
Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Wanandoa mashuhuri Kelvin ‘Bahati’ Kioko na Diana Marua walichagua njia maalum za kusherehekea mwana wao wa kulea Morgan Bahati ambaye aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya 14 mwezi uliopita.

Morgan ambaye amekuwa akiishi na wanandoa hao tangu kuchukuliwa kutoka kwa nyumba ya watoto ya ABC alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Desemba 22 na familia ya Bahati ilimuandalia karamu nzuri ambapo walimminia upendo, zawadi na maua.

Katika chapisho la siku ya Jumanne, Diana Marua alifichua kwamba mwanawe wa kulea alipata noti za pesa zilizowekwa kwenye maua kama zawadi ya nne, jambo ambalo lilimfurahisha sana.

“Zawadi namba 4 kati ya 5!!! Hii ilimfanya mvulana wa kuzaliwa kuwa na hisia sana. Lakini je, alikuwa tayari kwa zawadi namba 5?,” Diana Marua aliandika chini ya video ya Morgan akipokea pesa kutoka kwa kadi ya siku ya kuzaliwa iliyowekwa ndani ya shada la maua.

Katika video hiyo, mvulana huyo mwenye umri wa miaka 14 alionekana kushangaa na kufurahishwa sana alipopata pesa zile kutoka kwa maua hayo.

“Oh Mungu wangu! Nini! Ninaota?" alisema Morgan huku akiutazama mkanda wa pesa alizopewa.

Pia alisoma maandishi kwenye kadi iliyoambatanishwa na pesa hizo.

"Wewe ni baraka kubwa zaidi katika maisha yetu. Hujui jinsi ulivyotufanya tujivunie. Leo unatimiza miaka 14. Mwaka moja zaidi, mwenye busara zadi, mwenye nguvu zaidi. Matamanio yetu ni kwamba kila hitaji la moyo wako litimie na Mungu atujalie afya njema tukusherehekee maisha yako yote. Siku ya kuzaliwa yenye furaha na upendo mwingi. Kutoka kwa baba, mama, Mueni, Heavy, Majesty, Laishia na Joshua,” Soma ujumbe huo.

Kufuatia upendo alioonyeshwa na jamaa zake, kijana huyo alikiri kuwa hata alikuwa amepoteza maneno ya kutoa shukrani zake kwa familia ya Bahati.

"Mwaka wa 2023, imekuwa muda mrefu sana tangu kila mtu akusanyike kunisherehekea. Imekuwa ngumu sana, kichwani mwangu kuna mambo mengi..” Alisema Morgan kabla ya kuzidiwa na mihemko na kushindwa kuendelea na hotuba yake.

Pia alitumia fursa hiyo kumshukuru mwimbaji Bahati kwa kumtunza na kubainisha kuwa hangeweza kufika mbali alionao kama si yeye.

View Comments