logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ukileta ujinga nakuroga!" Nyota Ndogo amuonya mumewe mzungu dhidi ya kumuacha

Aliendelea kumhakikishia mzungu huyo kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na kuahidi kutomuacha kamwe.

image
na Samuel Maina

Burudani27 January 2024 - 07:58

Muhtasari


  • •Nyota Ndogo alibainisha kuwa mzungu huyo ndiye mshirika wake wa maisha aliyeteuliwa na akamshukuru kwa kumkubali pamoja na watoto wake.
  • •Aliendelea kumhakikishia mzungu huyo kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na kuahidi kutomuacha kamwe.

Mwimbaji mkongwe wa Kenya Mwanaisha Abdalla almaarufu Nyota Ndogo mnamo siku ya Ijumaa alimsherehekea mumewe kwa ujumbe mzuri na wa kusisimua alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, mama huyo wa watoto wawili alichapisha picha yake na mumewe Henning Nielsen na kutumia chapisho hilo kumsherehekea mzungu huyo kwa kuwa katika maisha yake.

Katika ujumbe wake, alibainisha kuwa raia huyo wa Denmark ndiye mshirika wake wa maisha aliyeteuliwa na akamshukuru kwa kumkubali pamoja na watoto wake.

“Ubavu wangu wa pili ni wewe, wewe ndio MUNGU aliniandikia. Uliamua utanipokea na wanangu ukanipokea nilivyo, yani unasemaga ukiwa na mimi huboeki,” Nyota Ndogo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliendelea kumhakikishia mzungu huyo kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na kuahidi kutomuacha kamwe.

Aidha, mwimbaji huyo mzaliwa wa Pwani aliapa kwa kejeli kumroga mume ikiwa atafikiria kugura ndoa yao.

“Mume wangu nakupenda sana, labda uniwache wewe lakini mimi siwezi kukubali kukupoteza. Ukileta ujinga nakuroga unarudi kwa laini,” aliandika,

Aliongeza ,”Kheri ya siku ya kuzaliwa mume wangu Henning. Wapendwa,. hii kitu imenishinda kujieleza kidhungu, munaweza ku translate akija asome vizuri aelewe. Haya wasomi njooni.

Nyota Ndogo na Bw Henning Nielsen wamekuwa kwenye ndoa ya mbali kwa takriban miaka sita. Wanandoa hao wawili walifunga pingu za maisha mwezi Mei 2016 baada ya kuchumbiana kwa muda.

Mapema mwaka jana Nyota Ndogo alifichua kuwa  ilichukua mwaka mmoja kwa yeye kujibu ombi la ndoa la mumewe huyo mzungu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved