logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya rapa Scar kupendekeza wanawake waolewe mapema ili kukomesha mauaji

Scar alisema njia mojawapo ya kupunguza mauaji ya wanawake ni kuwahimiza wasichana waolewe kabla ya kufikisha miaka 23.

image
na Samuel Maina

Burudani28 January 2024 - 10:21

Muhtasari


  • •Scar alisema njia mojawapo ya kupunguza mauaji ya wanawake ni kuwahimiza wasichana waolewe kabla ya kufikisha miaka 23.
  • •Pendekezo la Scar lilipokewa kwa hisia tofauti, baadhi wakionekana kumuunga mkono huku wengine wengi wakimkosoa.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameendelea kutoa maoni kufuatia pendekezo tata lililotolewa na rapa maarufu Scar wa kundi la Wakadinali kuhusu jinsi ya kupunguza visa vya mauaji ya wanawake vilivyokithiri nchini Kenya.

Katika taarifa yake Jumamosi jioni, Scar alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kupendekeza kwamba njia mojawapo ya kupunguza mauaji ya wanawake ni kuwahimiza wasichana waolewe kabla ya kufikisha miaka 23.

Scar alidai kuwa kwa kuolewa mapema, wanawake watawajibika kwani ni nadra wanawake walioolewa kukutana na wanaume wengine kwenye vyumba vya kulala wageni au kutembelea maeneo ya burudani.

"Njia mojawapo ya kupunguza mauaji ya wanawake ni kuwashauri wanawake wetu kuolewa wakiwa na umri wa miaka 23," Scar alisema kupitia Instastori yake.

Aliongeza, "Wanawake walioolewa hawaendi kwenye Airbnb na vilabu mara mingi. Hii sio sayansi ya roketi, come on #RongRende.”

Katika taarifa nyingine kwenye Twitter, alitoa wito wa kukomeshwa kwa mauaji ya wanawake ila pia akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa vijana kufundishwa umuhimu wa mapenzi.

Pendekezo la Scar hata hivyo lilipokewa kwa hisia tofauti na wanamtandao wa Kenya, baadhi wakionekana kumuunga mkono huku wengine wengi wakimkosoa.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii;-

Kassim Lutta: Let us educate our children to grow up knowing that life is sacred..and it's only God who can take it away..and at the same time to know that there is no short-cut in good life.

Nginga: Solution ni kufunza watoto waache tamaa hakuna cha rahisi kama vile zamani watu waliishi kufunzwa shule nyumbani na kanisani

@RealRonaks: People are avoiding or missing the part of “one way of reducing femicide…”. Kenyans we have a long way to go.

@tsuro25: More women are murdered by their husbands, in their homes, whilst pregnant. You are an idiot.

@felixnewkid: Amesema one way sio only way, tulieni.

@ziggy_hynis: Ati marry? How will frustrated broke and idle men take care of a woman? Itakuwa tu ni vita na mauaji tu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved