In Summary

•Miracle Baby ameapa kwamba akitoka hospitali atakuwa mhubiri. Mwanamuziki huyo amekuwa hospitali kwa muda mrefu. 

•Mpenzi wake Carol Katrue aliomba mashabiki wao kwenye  mitandao ya kijamii wamuweke msanii huyo kwa maombi.

Miracle Baby
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Gengetone na Mugithi  Peter Mwangi anayejulikana kama Peter Miracle baby ameapa kwamba akitoka hospitali atakuwa mhubiri. Mwanamuziki huyo amekuwa hospitali kwa muda mrefu. 

"Bwana asifiwe, nikitoka hapa ntakua pastor, na nitahubiri neno la Mungu"

Takriban wiki moja iliyopita alifanyiwa upasuaji wa tatu  mnamo Jumanne, Februari 6.

Mpenzi wake Carol Katrue aliomba mashabiki wao kwenye  mitandao ya kijamii wamuweke msanii huyo kwa maombi.

"Anaenda kufanyiwa upasuaji wa tatu, tunahitaji maombi yenu," Katrue aliandika kwenye picha ya Miracle baby aliyeonekana akiwa mdhaifu.


miracle baby,

Baadaye alieleza mashabiki kuwa upasuaji uliendelea vizuri na akashukuru kila mtu aliyeweka Miracle  Baby kwa maombi na kuwaomba wazidi kumwombea.

"Asante Mungu kwa upasuaji uliofaulu lakini endeleeni kumuombea," Katrue aliandika kwa Instagram stories.

Aliendeleza na kueleza kuwa Miracle baby alifanyiwa upasuaji kutokana na kupasuka kwa utumbo.

Siku 2 zilizopita, Katrue aliandika tena kwa mtandao kwamba anaomba mashabiki waoa wawasaidie kukusanya milioni 1.6 ya kulipa bili ya hospitali.

" Miracle Baby anatolewa hospitali kesho na tunaomba mtusaidie kulipa bili ya hospitali yenye sai imefika  milioni 1.6. Mnaeza tuma mchango wenu kwa number yangu  0794790255 ", Katrue aliandika kwa mtandao,Instagram.
View Comments