In Summary
  • Alai aliandika katika kwa mtandao wake wa kijamii wa X (Twitter) kwamba Mungai Eve anastahili kushtaki Trevor kwa kubadilisha jina la kampuni na kumvuta Mungai Eve kazi.
Trevor na mpenzi wake Mungai Eve
Image: Instagram

Robert Alai amemtetea Mungai Eve na kumshauri kushtaki aliyekuwa mpenzi wake Director Trevor na kuenda kinyume na msimamo wa awali kuhusu umiliki wa mitandao akitengana na yeye.

Jumatatu jioni, Director Trevor ambaye jina lake halisi ni Bonaventure Monyancha alitangaza mabadiliko katika kampuni ya Mungai Eve Media.

Alifichua kuwa kutakuwa na mabadiliko kwenye chaneli za YouTube za Mungai Eve na Insta Fame zenye jumla ya wafuasi zaidi ya 850,000 pamoja na ukurasa wa Facebook wa Mungai Eve Media wenye takriban wafuasi 874,000.

Jambo hili halikuwafurahisha watu wengi mmoja wao akiwa Robert Alai ambaye ni mwanablogu. 

Alai aliandika kwa ukurasa wake wa X (Twitter) kwamba Mungai Eve anastahili kumshtaki Trevor kwa kubadilisha jina la kampuni na kumfuta  kazi.

Katika sehemu ya maoni, ilionekana kuwa watu wengi hawakubaliani na bwana Alai. Wengi wao walikuwa wanatetea Director Trevor na kusema kuwa ana haki sawa katika kampuni hiyo.

Trevor alieleza kuwa waliachana na mpenzi wake Mungai Eve February 23 mwaka wa 2023 lakini walibaki kuwa marafiki na  washirika wa biashara mpaka wakati ambapo alisema kuwa hataki kufanya kazi tena na kampuni hiyo.

Katika video ya kitambo ambayo alihojiwa na mwanahabari mwenzake wa YouTube, Presenter Ali alikuwa ameulizwa jinsi uhusiano wao wa kikazi ungeendelea ikizingatiwa kuwa Eve ndiye aliyekuwa mhoji huku Trevor akichukuwa video.

Trevor alijibu kuwa ""Huyu ni dame. Mi ndio najua.  Mimi ndio nilicreate channel lakini ni yake."

Aliendelea na kusema, "Labda kukiwa na masuala ningependa iwe yake. Mimi naeza anza channel leo na bado iwe freshi kabisa. Kwa sababu brand ni yake, jina ni lake. Hata saa hii habari zote ni zake. Mimi najua tu password. Mambo mengine sijui. Mambo ya hela sijui."

Licha ya Trevor kutangaza maendeleo mapya, Mungai Eve bado hajazungumza kuhusu madai hayo.

View Comments