logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta Ezekiel anaeleza sababu za idadi ya juu vya vifo miongoni mwa vijana

Pasta Ezekiel Odero amezungumzia wasiwasi mkubwa wa vifo vya mapema vya vijana wengi.

image
na Davis Ojiambo

Burudani20 March 2024 - 09:32

Muhtasari


  • Alisema kwamba vijana wadogo wananaswa bila kujua katika mtandao wa giza, ambapo maisha yao hutumiwa kama matoleo.
mchungaji Ezekiel Odero

Mwanzilishi wa kanisa la New Life Prayer Centre mhubiri  Ezekiel Odero ameelezea hofu kuhusiana na vifo vya mapema vya vijana wengi nchini Kenya.

Kulingana na mchungaji Ezekiel, vifo hivi sio vya kawaida na na kuvihusisha na utoaji kafara.

Alisema kwamba vijana wadogo wananaswa bila kujua katika mtandao wa giza, ambapo maisha yao hutumiwa kama matoleo.

"Unaona vifo hivi vinavyowapata vijana wa kiume, vinahusishwa na viapo na mila. Jinsi wanavyojiua ni kuhusu hili. Mimi huwa nawaambia kuwa mtandao ni kitu kizuri, lakini ni kikubwa kuliko ulimwengu huu. Chagua mahali pa kuishi kwenye mtandao kwa sababu huwezi kuishi kila mahali kwenye mtandao."

Katika ombi lake Mchungaji Ezekiel aliwahimiza vijana kumgeukia Mungu na kutafuta kimbilio katika ufalme wake.

Alionya dhidi ya kuvutia kwa mtandao, akisema kuwa inaenea zaidi ya ulimwengu wetu wa kimwili.

"Vijana, mgeukieni Mungu. Nje ni mbaya. Vifo hivi vingi vinapaswa kutupa changamoto ya kumrudia Mungu. Hatuwezi kufa tu hivyo. Watu wanawatolea wengine dhabihu kwa madhabahu wanayotumikia. Ni dhabihu tu. Sio vifo vya kawaida. Wanaambiwa watoe dhabihu watu wanaowapenda zaidi. Na kwa sababu ya nguvu mbaya, kesi zao kawaida huisha bila haki", alisema mchungaji Ezekiel.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved