In Summary

• Mulamwah ameonyesha screenshot ya anayodai kuwa ni salio lake la benki, ikionyesha kuwa amebakisha Sh66.17 pekee.

•Chapisho hilo limezua hisia mseto, baadhi wakimuonea huruma, wengine wakidai si kweli huku wengine wakimdhihaki.

Mulamwah na mpenzi wake Ruth baada ya kununua gari
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah ameonyesha screenshot ya anayodai kuwa ni salio lake la benki, ikionyesha kwamba amebakisha Sh66.17 pekee.

Kulingana na baba huyo wa watoto wawili, hizo ndizo pesa pekee zilizosalia katika akaunti yake ya benki baada ya kununua gari aina ya Mercedes Benz mapema wiki hii.

Mulamwah amedai kuwa ataanza upya kuweka akiba baada ya ununuzi wa gari kumuachakaribu  bila chochote katika benki.

“Bank balance baada ya benzo, tunaanza fresh, yako ni ngapi?” Mulamwah aliandika chini ya picha ya skrini ya kile alichodai ni salio lake la benki.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Chapisho hilo limezua hisia mseto kutoka kwa wanamtandao, wengine wakimuonea huruma, wengine wakidai si kweli huku wengine wakimdhihaki.

@babushkakenya: Izah joh kuja nikujazie tank uanzie life bro! Nil life.

moohnjeri: Leta account number nikuwekee kakitu baba keilah.

commentator_254: nitumie hio bro.

kenya.gossip.club: Uongo

jkuria361: Ya fuel ulipewa na kampuni ama?

Mulamwah alifichua habari za fanikio hilo lake kubwa siku ya Alhamisi wakati ambapo alishiriki picha za gari zuri aina ya Mercedes Benz E250 alilonunua.

 

Wakati akitoa tangazo hilo, mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alimshukuru Mungu, familia yake na mashabiki kwa jukumu muhimu walilocheza katika mafanikio hayo.

“MUNGU ALIFANYA 💪🙏 mmiliki gari mwenye fahari 💯 mercedes BENZ E250 innit . kila mara tembea polepole lakini, sogea ipasavyo 💯. namshukuru Mungu kwa baraka zote maishani, wacha tuanzie ka life apa . shukrani kwa familia, mashabiki na marafiki kwa usaidizi wenu na maombi kila mara,” Mulamwah alisema.

Baba wa watoto wawili alidokeza kuwa gari hilo sasa litamsaidia mzazi mwenzake Ruth na mtoto wao mdogo kusafiri hadi kliniki kwa urahisi kila inapohitajika.

Pia hakusahau kumshukuru mpenzi wake kwa sapoti ambayo ameendelea kumpa.

 “Kijana cha kitale sasa ni former pedestrian. kalamwah na mama kalamaz clinic wanafika in style sasa . @atruthk asante kwa support daima mamake,” alisema.

Mpenzi wake Ruth K, kwa upande wake alimsherehekea kwa kununua gari hilo maridadi na kumpongeza kwa mafanikio hayo.

"Hongera baba Kalamwah," Ruth K aliandika chini ya video yake akiwa amesimama kando ya gari nyeusi aina ya Mercedes.

Alibainisha kuwa Mulamwah anastahili sana gari hilo akifichua kwamba ilimchukua bidii, maombi na kujitolea kulinunua.

"Matokeo ya uvumilivu, maombi, bidii na kujitolea🎉🎉 hongera baba kalamz @oyando_jnr kwa ushindi huu♥️," aliandika.

Aliongeza, "Hii ni ya thamani ya kusubiri , Nisaidieni kumpongeza mmiliki mpya wa gari mjini🎉♥️anastahili sana. Ninafurahi na kujivunia wewe sana, nakupenda♥️.Road test unanipelek#a wapi🙈😋

Mama huyo wa mvulana mmoja pia hakuweza kuficha jinsi anavyojivunia mpenzi wake.

View Comments