Shabiki wa reggae Stephen Bhingi amechapisha ujumbe mtamu kwa Mungai Eve huku akionyesha mapenzi yake kwake.
Wakati wa mahojiano na Mungai Eve, Bhingi alikiri kwa ucheshi kumpenda, na hivyo kuibua kicheko kutoka kwa Youtuber huyo.
Kwa sauti nyepesi, Bhingi alimhakikishia Mungai kwamba urefu wake haufai kuwa kizuizi, akisisitiza nia yake ya kutimiza madhumuni yao duniani.
"Ni kugonga upate mtoto.Jah alitucreate akasema tufulfil the dunia. Kwa hivyo tunafaa kufufil dunia, kujaza kujaza dunia,"alieleza.
Mwingiliano wao ulichukua mkondo wa kuchekesha pale Bhingi alipomfananisha Mungai na mpenzi wake wa zamani, jambo lililozua kicheko kutoka kwa wote wawili.
"Unajua, wewe ni mfupi", She remarked to which Bhingi replied, "ili mradi we ni mrasta, we unacheza na rada, juu ukicheza na rada, si unajua as long as we hauna pressure...".
Bhingi anayejulikana kwa mtindo wake wa maisha ya rasta, amejikusanyia wafuasi wengi kwenye TikTok, ambapo anashiriki vijisehemu vya maisha yake.
Katika chapisho la hivi majuzi, alinukuu maudhui yake na ujumbe wa shukrani kwa Jah Aliye Juu Zaidi.
Bhingi alikuwa katika vichwa vya habari hivi majuzi kwa mkutano wake na rais William Ruto, na kuzua shauku ya Wakenya kuhusu mjadala wao.
Alikuwa miongoni mwa wageni walioalikwa kushuhudia tangazo la uhamasishaji wa maudhui kwenye Facebook, reel, na Instagram wakati wa mkutano wa Rais na Timu ya Usimamizi wa Facebook katika Ikulu ya Nairobi.