In Summary

•Nyaboke Moraa aliomboleza binti yake katika chapisho la kwanza la mtandao wa kijamii tangu kifo chake cha kusikitisha.

•Blak Aende aliandika kumbukumbu fupi na ya kihisia akisema kwamba Jumapili ilikuwa moja ya siku mbaya zaidi maishani mwake.

Blak Aende na Nyaboke Moraa wamemuomboleza binti yao Marie Achieng

Muigizaji na mchekeshaji maarufu wa Kenya, Gloria Nyaboke Moraa, na mzazi mwenzake Blak Aende wameomboleza kifo cha binti yao wa miaka 19.

Marrie Achieng, ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Nyaboke Moraa alipoteza maisha katika hali isiyojulikana mnamo Jumapili, Julai 28.

Siku ya Jumatatu, muigizaji huyo mahiri aliomboleza binti yake katika chapisho la kwanza la mtandao wa kijamii tangu kifo chake cha kusikitisha.

"Nitaanzia wapi?" Nyaboke Moraa alisema kupitia mtandao wa Facebook.

Pia alichapisha video ya kumbukumbu iliyomuonyesha akicheza dansi na marehemu binti yake na kuiambatanisha na emoji ya mapenzi.

Siku hiyo hiyo, mzazi mwenza wa Bi Moraa, mfanyabiashara Blak Aende pia aliomboleza kifo cha binti yao Marrie Achieng.

Blak Aende aliandika kumbukumbu fupi na ya kihisia kwa binti yake akisema kwamba Jumapili ilikuwa moja ya siku mbaya zaidi maishani mwake.

"Ni Siku ya giza. Siwezi kumhoji Mungu, ninamwachia kila kitu (Mungu)," Blakaende aliandika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Baadaye aliweka chapisho lingine likimuonyesha akiwa ndani ya ndege akisafiri nyumbani na juu yake akaandika, "Safari ya ndege ngumu zaidi kuchukua," ikisindikizwa na emojis za moyo mweusi.

Kifo cha Marrie kilitangazwa Jumapili jioni na muigizaji rafiki wa karibu wa Moraa, Sandra Dacha.

"Ni kwa masikitiko makubwa ninawatangazia kuaga kwa binti ya @nyabokemoraa. Maombi yako ndio anayohitaji kwa sasa🙏🏿Pumzika kwa amani Marrie😭," Sandra aliandika.

Sababu ya kifo cha Marrie bado haijawekwa wazi. Alikuwa na umri wa miaka 19 wakati wa kifo chake.

View Comments