In Summary

•Faizah ambaye ni binti ya Patiz na mpenzi wake Eunice Wambui alipoteza maisha mnamo Septemba 14, 2024 baada ya kuugua.

•Baby Faizah ambaye alikuwa na umri wa miezi michache tu alipoteza maisha ghafla mnamo Septemba 14.

DJ Patiz na mpenziwe Eunice Wambui walimzika mtoto wao mnamo Septemba 17, 2024.
Image: HISANI

Baby Faizah, binti ya mcheza santuri maarufu wa reggea DJ Patiz, alizikwa siku ya Jumanne Septemba 17 baada ya kufariki siku chache zilizopita.

Faizah ambaye ni binti ya Patiz na mpenzi wake Eunice Wambui alipoteza maisha mnamo Septemba 14, 2024 baada ya kuugua.

Msichana huyo mchanga alizikwa nyumbani kwao siku ya Jumanne na DJ huyo wa reggea ameelezea wasiwasi wake kuhusu jinsi atakavyopona kutokana na msiba huo..

“Leo tumemlaza Mtoto Faizah. Mimi sijui nitarecover aje kutokana na hili,” DJ Patiz aliandika kwenye mtandao wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha yake na mzazi mwenzake Wambui wakiweka maua juu ya kaburi la binti yao.

“Wewe jua utaishi kwa roho yangu milele na daima, hadi tukutane tena mtoto wa mfalme,” aliongeza.

Baby Faizah ambaye alikuwa na umri wa miezi michache tu alipoteza maisha ghafla mnamo Septemba 14. Sababu halisi ya kifo haijafichuliwa hadharani.

Wakati akitangaza habari za kusikitisha za kifo cha bintiye, DJ Patiz aliitakia roho ya msichana huyo mchanga amani inapopumzika.

"Septemba 14 iliniibia ulimwengu wangu. Hata kifo siku moja kitakufa, angaza njiani Baby Faizah,” DJ Patiz alitangaza.

Katika chapisho lingine, alionyesha picha nzuri akiwa amemshika msichana huyo na kusimulia jinsi bintiye alivyokuwa na afya njema siku moja kabla ya kifo chake.

“RIP my little girl Baby Faizah, nitaelezea watu aje hii ni picha ya jana tu ukiwa mwenye nguvu?? Hii nayo imeniuma sana,” alisema.

Hafla ya kuwasha mishumaa ilifanyika mapema wiki hii kusherehekea maisha ya msichana mdogo aliyezaliwa Mei mwaka huu.

View Comments