In Summary

• Akothee alionyeshaa vyeti vyake vya masomo alipokuwa akizungumzia safari yake ya elimu yenye changamoto.

•alifichua kwamba alifanya mitihani yake ya KCSE mwaka wa 2004 katika Shule ya Sekondari ya Wasio Mixed na kupata alama ya C+.

Akothee alihitimu Desemba 2023.
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Jumamosi jioni, mwimbaji na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee alionyeshaa vyeti vyake vya masomo alipokuwa akizungumzia safari yake ya elimu yenye changamoto.

Katika chapisho lake kwenye ukurasa wake wa Facebook, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alifichua kwamba alifanya mitihani yake ya KCSE mwaka wa 2004 katika Shule ya Sekondari ya Wasio Mixed na kupata alama ya C+.

Akothee alipata C plain katika Kiingereza, B- katika Kiswahili, D+ katika Hisabati, B plain katika Biolojia, C- katika Kemia, A katika Historia na B- katika Biashara.

Mama huyo wa watoto watano pia alionyesha cheti chake cha digrii kutoka Chuo Kikuu cha Mount Kenya ambako alisomea Shahada ya Usimamizi wa Biashara (Human Resource Management) na kupata Second Class Upper Divison.

Wakati akizungumzia safari yake ya elimu, alifichua kwamba wakati wa siku zake za kwenda shule, wakati fulani aliona elimu kuwa mzigo. na hakutambua thamani yake. Alifichua kuwa wakati fulani akiwa katika shule ya Sekondari hata alitoroka nyumbani kwake ili aende kuolewa.

"Kuacha masomo katika kidato cha pili na kuchagua ndoa ilionekana kuwa njia, lakini maisha yalikuwa na mpango tofauti. Ndoa ilileta changamoto, lakini pia kuweza kutambua kuwa elimu yangu haikukamilika.

Kwa uzito wa majukumu, nilirudi nyuma, nikiwatanguliza watoto wangu, ndugu na dada zangu, na familia yangu juu ya matarajio yangu mwenyewe. Mapambano yaliendelea hadi uhuru wa kifedha ukawa ukweli wangu," Akothee alisema.

Mwanamuziki huyo alifichua kwamba alijaribu kuendeleza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Tawi la Mombasa mwaka wa 2007 lakini uhaba wa kifedha ulimlazimu kuahirisha masomo yake. Ilikuwa hadi 2013 alipofanikiwa kujiandikisha katika Chuo Kikuu cha Mount Kenya na kufanya digrii yake.

“Anasa hazikujaza utupu; elimu ilidumu kama matarajio yasiyotimizwa. Kwa kutambua uwezo wangu, nilielekeza upya mtazamo wangu. Leo, ninasimama kama ushuhuda kwamba bado hujachelewa. The Birth of Akothee Academy inaashiria safari yangu - kutoka kwa mapambano hadi ushindi," alisema.

Pia alitumia fursa hiyo kuwahimiza wale waliositisha safari yao ya elimu kwa sababu mbalimbali kurejea shuleni na kuchukua walikotoka.

View Comments