logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alinipata nikiwa maskini na kunitunza kama mtoto wake,'Zuchu amshukuru Diamond Platnumz

Ni msanii ambaye ana uhusiano wa karibu na mwema na Diamond, kama inavyoonekana mitandaoni.

image
na Radio Jambo

Burudani01 December 2021 - 09:30

Muhtasari


  • Ni msanii ambaye ana uhusiano mwema na wa karibu na Diamond, kama inavyoonekana mitandaoni
  • Licha ya kejeli zote ambazo Zuchu amepokea kutoka kwa wanamitandao, amezidi kutia bidii kila kuchao
Zx8k9kpTURBXy85MTIwMjZjODUzZGJhOGRlODA3NjhiNTVmNzFkNzBjNS5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE

Msanii Zuchu ni miongoni mwa wasanii ambao wamesajili katika lebo ya WCB inayomilikiwa na staa wa bongo Diamond Platnumz.

Baada ya kujiunga na lebo hiyo Zuchu ameonekana akiinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kutokana na biii yake.

Ni msanii ambaye ana uhusiano mwema na wa karibu na Diamond, kama inavyoonekana mitandaoni.

Licha ya kejeli zote ambazo Zuchu amepokea kutoka kwa wanamitandao, amezidi kutia bidii kila kuchao.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo alipakia video huku akionyesha nyumba yake na kusema kwamba alikuwa ameithamini.

Pia aliweka wazi kwamba yuko tayari kusherehekea sikukuu ya krismasi, na hata kumshukuru Diamond kwa umbali amemtoa.

" Mimi Dai akinipata sikuwa na chochote . Alinikuta maskini akanitunza kama Mtoto wake. Alinipa mkataba katika Lebo yake, akanipa nyumba , akanipa gari na kunitafutia umaarufu unaonilisha Leo hii. Dai ni zaidi ya babangu Allah azidi kumueka poa Kwa ajili ya wengine wengi," Alisema Zuchu.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved