logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chris Brown azungumza baada kushtakiwa kwa ubakaji

Mwanamziki wa mtindo wa RnB ameweka hadharani na kuzungumzia madai yanayomhusisha na kumbaka mwanamke mmoja kwa jina Jane Joe.

image
na Davis Ojiambo

Burudani31 January 2022 - 05:56

Muhtasari


  • • Mwanamziki wa mtindo wa RnB ameweka hadharani na kuzungumzia madai yanayomhusisha na kumbaka mwanamke mmoja kwa jina Jane Joe.
  • • Katika hati za mahakamani zilizofichuliwa na wadadisi wa vyomnbo vya habari nchini Marekani, hati hizo zinaeleza kuwa mwanamke huyo anadai kuburuzwa na kubakwa na mwanamuziki huyo kwenye jahazi huko Florida mwishoni mwa mwaka 2020

Mwanamuziki wa mtindo wa RnB amejitokeza na kuzungumzia madai yanayomhusisha na kumbaka mwanamke mmoja kwa jina Jane Joe.

Katika karatasi za mahakamani zilizofichuliwa na wadadisi wa vyombo vya habari nchini Marekani, hati hizo zinaeleza kuwa mwanamke huyo anadai kuleweshwa na kubakwa na mwanamuziki huyo kwenye jahazi huko Florida mwishoni mwa mwaka 2020

Katika kile kinachoonekana kama kujitetea, mwanamuziki Chris Brown ameandika, "natumai nyinyi wote mnaona muundo na mtindo huu, kila ninapoachia kazi, muziki na miradi yangu, watu wanajaribu kuvuta ujinga wa kikweli."

Karatasi za mahakamani zinaonesha kuwa  mwanamke huyo anayemshtaki Brown kwa madai ya ubakaji ni mtaalam wa kusakata densi, mwanamitindo na msanii wa muziki pia.

Katika kesi hiyo, mwanamke  Jane anadai alialikwa kwenye jahazi na mwanamuziki huyo ambaye baadaye alimtaka waelekee katika nyumba moja kisiwani Star haraka iwezekanavyo.

Punde baada ya kufika katika nyumba hiyo, Jane anasema alikaribishwa jikoni na kupewa kinywaji kwa kikombe cha rangi nyekundu huku mwanahabari huyo akimpa mawaidha jinsi ya kunawiri ndoto yake kimuziki.

katika maongezi hayo, mwanamuziki Chris Brown inadaiwa alimzidishia kinywaji kikombeni mwake kwa mara kadhaa mpaka alipoanza kuhisi kutokuwa imara na kuanza kupotea katika usingizi.

Ni wakati huu mwanadada huyo anadai Brown alimchukua kitandani mwake na kumtendea unyama huo wa ubakaji.

"Chris Brown alichukua simu yangu na kujitumia arafa ili kupata namba yangu. kesho yake alfajiri alinitumia ujumbe mfupi akanitaka nimeze vidonge," sehemu ya hati hiyo ya mahakama ilisoma.

Katika kesi hiyo, Jane anadai Brown kumlipa kima cha milioni $20 kama fidia kwa dhiki kali za kihisia, udhahirisho wa kimwili, uchungu wa kihisia, hofu, wasiwasi, fedheha, huzuni na majeraha mengine ya kimwili miongoni mwa madai mengine.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved