logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nina wivu, natamani niwe tajiri kama Diamond- Esma Platnumz afunguka

Esma alisema wivu wake kwa utajiri wa Diamond ndio unaomfanya ajitume zaidi kazini.

image
na Radio Jambo

Makala08 June 2022 - 08:36

Muhtasari


•Esma alisema wivu wake kwa utajiri wa Diamond ndio unaomfanya ajitume zaidi katika biashara yake ya nguo.

•Alisema hawezi kufikiria kutegemea utajiri wa Diamond maishani kwa kuwa ni jambo ambalo linaweza kumletea dharau.

Esma Platnumz na Diamond Platnumz

Mfanyibiashara Esma Platnumz amefichua kwamba huwa anatia bidii kubwa sana katika kazi yake kwa sababu anatamani sana kuwa tajiri kama kaka yake Diamond.

Akiwa kwenye mahojiano na Global TV, Esma alisema wivu wake kwa utajiri wa Diamond ndio unaomfanya ajitume zaidi katika biashara yake ya nguo.

"Mimi natamani niwe kama Naseeb. Sio eti niwe mwanamuziki lakini natamani yale maendeleo yake. Ili niwe kama yeye ni kujituma kwa bidii," Esma alisema.

Mama huyo wa watoto wawili aliweka wazi kuwa kamwe hawezi kujibweteka eti kwa kuwa kaka yake ni tajiri mkubwa.

Alisema hawezi kufikiria kutegemea utajiri wa Diamond maishani kwa kuwa ni jambo ambalo linaweza kumletea dharau.

"Unapomuona mwenzio tajiri nawe unatamani kuwa kama yeye. Kutamani kuwa kama yeye ni kufanya kazi kwa bidii. Sio kwa sababu eti ndugu yako tajiri eti ujibweteke, kwanza utadharaulika. Wafanyikazi wake na watu wa karibu pia watakudharau. Utafikia mahali ambapo ata mbwa wake watakudharau," Alisema.

Esma alisema kwamba huwa anapendelea kuwa katika duka lake la nguo kwa kuwa wateja wake wengi hupenda awahudumie mwenyewe.

Pia alifichua kuwa Mama Dangote huonekana pale mara nyingi kwa kuwa yeye sio mzazi tu bali pia ndiye rafiki yake mkubwa.

"Yeye ndiye rafiki yangu aliyekuwepo. Mimi sinanga marafiki. Marafiki wengine huja na mambo zao," Alisema.

Mfanyibiashara huyo alisema alimchagua Mama Dangote kuwa rafiki yake kwa kuwa huwa anasapoti kazi yake kwa dhati.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved