Mwanasoshalaiti Huddah Monroe amewakashifu kina mama wadogo ambao wanaenda kujivinjari katika vilabu miezi michache tu baada ya kujifungua.
Kulingana na Huddah, hilo ni thibitisho kuwa mama huyo hana mapenzi ya dhati kwa mtoto wake mchanga.
Huddah alidai kwamba sababu pekee inayoweza kufanya mwanamke aliye na mtoto kupatikana katika kilabu ni ikiwa anafanya kazi pale au kuuza bidhaa mle ndani kwa mnajili ya kujipa kipato cha kulea mtoto wake.
''Coz Chille jinsi watu wanavyozaa na kukimbilia vilabu inashangaza. Pata mtoto kama uko tayari kulea na kuonyesha mtoto mapenzi ya dhati,mnawawacha na akina nani ?'' Huddah aliuliza.
Huddah pia aliwashauri wasichana kuwa makini na wanaume ambao wanaoshiriki tendo la ndoa nao kwani baadhi yao hawapendi kuwajibika pindi wanapopachika mimba.
''Inafaa ujilinde vizuri inapofika katika maswala ya kimapenzi, makahaba ndo hawajali kujilinda anatoka na kila mtu, kama wewe ni mmoja wao na hiyo ndo namna unapata riziki yako basi tutakuelewa, lakini jilinde usipate mtoto mapema''Huddah alisema.
Mwanasosholaiti huyo amebainisha kuwa haapendi kuona watoto wakihangaika na hataki mama yeyote kumdharau mtoto wake.