logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ujumbe wa Amber Ray kuhusu maisha yake ya awali wazua gumzo

Pia alifichua kwamba alifanya makosa ambayo aliomba msamaha

image
na Radio Jambo

Yanayojiri01 August 2022 - 16:29

Muhtasari


  • Kulingana na Amber awali alimuasi Mungu, na kuwakosea wengi bali hayo hayamzuii kuishi maisha yake ya sasa

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray amzua gumzo tena mitandaoni baaada ya kusimulia maisha yake ya awali.

Kulingana na Amber awali alimuasi Mungu, na kuwakosea wengi bali hayo hayamzuii kuishi maisha yake ya sasa.

Pia alifichua kwamba alifanya makosa ambayo aliomba msamaha, lakini  makosa yake ambayo alijifunza kwayo ndio yanamfanya aishi maisha yake.

Amber kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesema kuwa anafurahia maisha ambayo anaishi kwa sasa.

"Kitu ambacho siwezi kuwa na aibu nacho ni maisha yangu ya nyuma... nakubali nimefanya makosa mengi sana, nimevunja sheria nyingi sana, nikamuasi Mungu kwa njia nyingi na kuomba msamaha lakini siwezi kujizuia na maisha yangu ya nyuma coz ndivyo ilivyo. ilinifanya niwe hivi leo …sijui siku zijazo zimeniwekea nini lakini najua nyasi huwa kijani kibichi kila mara upande ule mwingine; na niko nafurahia sana awamu hii na siwezi kusubiri kuona ukuaji zaidi🄰 Asante mpenzi wangu kwa kukusudia."

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved