logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Amber Ray afunguka kuhusu kuchumbiana na mume wa hasidi wake, Vera Sidika

Mwanasosholaiti huyo amesisitiza kwamba hajawahi kuwa kwenye mahusiano na Mauzo.

image
na Radio Jambo

Makala23 March 2023 - 07:00

Muhtasari


•Amber Ray na Mauzo walidaiwa kuchumbiana miaka michache iliyopita baada ya picha zao pamoja kusambaa kwenye mitandao ya kijamii

•Mwanasosholaiti mwenzake Vera Sidika alikana madai ya 'kumwiba' mwanamuziki huyo mzaliwa wa pwani kutoka kwake.

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray amesisitiza kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano na mwimbaji Brown Mauzo.

Wawili hao walidaiwa kuchumbiana miaka michache iliyopita baada ya picha zao pamoja kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Huku akiwashirikisha mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram, Amber Ray hata hivyo alitupilia mbali madai ya kuchumbiana na mume huyo wa hasidi wake Vera Sidika.

"Je, kweli ulichumbiana na Mauzo au ilikuwa showbiz?" shabiki aliuliza.

Katika jibu lake, mpenzi huyo wa Kennedy Rapudo alisema kwamba kilichotokea kati yake na Mauzo ni biashara tu na akafichua kuwa hata hawakuwahi kubusu.

"Ilikuwa showbiz, hatujawahi hata kubusu," alisema.

Hapo awali, mwanasosholaiti mwenzake Vera Sidika alikana madai ya 'kumwiba' mwanamuziki huyo mzaliwa wa pwani kutoka kwake.

"Mume wangu alikuwa single nilipokutana naye, mimi pia nilikuwa single. Mwanamke huyo (Amber Ray) hajawahi kuwa na mahusiano naye. Ilikuwa biashara tu. Tulikuwa tunachumbiana wakati kiki inaendelea," Vera alisema kwenye Q&A.

Wiki iliyopita, wanasosholaiti hao wawili walihusika katika vita vya maneno kuhusu hafla ya kufichua jinsia ya mtoto. Vera alimshtumu Amber Ray kwa kuiga mtindo wake wa kufichua jinsia ya mtoto wake, madai ambayo mpenzi huyo wa Rapudo alijitokeza kuzungumzia na kuyakana baadaye.

“Kama malikia, napenda sana kuwahimiza watu kusema kweli, pia wao walikuwa wanataka kufichua jinsia ya mwanao kwa kutumia helikopta, mpaka pale nilipopakia yangu na ikatrend kwa siku tatu mitqandaoni. Baada ya hapo, walilazimika kutafuta njia mbadala kwa sababu wangetumia chopper ingeonekana kawaida sana kuwa wameniiga,” Vera alisema kwenye mtandao wa Instagram.

Vera alizidi kusema  Amber anamchukia kumuita mtu mbaya lakini wakati huo huo anazidi kumfuatilia na kutaka kuiga kila kitu anachokifanya.

“Nimejifunza kitu kimoja kwamba wabaya wako ni mashabiki wako ambao hawataki kukubali. Hakuna kitu kibaya katika kumhimiza mtu lakini ni vizuri wakati himizo hilo linakuja kutoka kwa sehemu nzuri. Na mimi siombi radhi katika hili kusema kweli,” alisema.

Kwa upande wake, Amber Ray alisema  wazo la kufichua jinsia ya mtoto si la Mkenya yeyote bali wote wanaliiga kutoka kwa mwanamke mmoja kwa jina Jenna Karvunidis aliyefanya hivyo mara ya kwanza mwaka 2008.

Alisema kwamba wote wanafichua jinsia ya watoto wao wajao si kuwaonesha watu kitu bali ili kujiridhisha wenyewe.

“Tunafanya karamu ili kufurahiya isiwe mtindo bora mitandaoni. Mchezo wangu ni wa asili, umaarufu wangu huja kwa kawaida ... kama vile ulivyofanya sasa. Kuwa mbunifu kufurahiya sio kuburudisha. Hebu starehe yako iwe burudani yao… Na Unikome tafadhali!!!” mwanasoshalaiti huyo alijibu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved