Seneta maalum Karen Nyamu Jumanne alipanda piki piki akielekea katika kikao cha kamati ya bunge.
Katika video aliyopakiwa kwenye akaunti yake ya Instagram, Karen alieleza kuwa kutokana na msongamano wa magari katika barabara ya Uhuru Highway jijini Nairobi alilazimika kutumia boda boda ili kutochelewa.
“Asubuhi ya leo nilikuwa nachelewa kufika kwenye kikao cha kamati ya ICT kwa ajili ya kuchunguza mswada vipengele zilizoko katika mswada wangu.” alieleza sababu ya kuabiri boda boda.
Katika video hiyo, seneta huyo alionekana kufurahia safari yake juu ya boda boda hiyo licha ya kulala mikia hali mbaya ya barabara hiyo ya piki piki.
Mbunge huyo aliwakilisha mswada mbele ya kamati ya bunge inahusiana na maswala ya kijiditali, mswada huo unapendekeza kufanya kuwa lazima kwa wanafunzi kufanya kozi za kidijitali.
Hili, kulingana na seneta huyo, litasaidia pakubwa katika kuwawezesha vijana kukidhi matakwa ya soko la sasa la ajira la kufahamu maswala ya kidijitali kwa umakini.
Seneta huyo mteuliwa pia anataka kutathminiwa kwa watumishi wote wa umma ili kuhakikisha kuwa wote wanafahamu maswala ya kidijitali.
"Tunahitaji wafanyikazi ambao wana ujuzi wa kidijitali ili kuongeza tija," seneta huyo alieleza.
Mwanasiasa huyo anakumbwa na utata mitandaoni kutokana na mahusiano yake ya kimapenzi na msanii wa nyimbo za Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh licha ya wawili hao kutokuwa katika ndoa rasmi.
Mwansiasa huyo kwa muda sasa wametupiana cheche za matusi mitandaoni na mke wa awali wa mwanamziki huyo, Edday Nderitu kwa kile kilichonekana ni mvutano wa nani mke bora kwa mwanamziki huyo.
Mapema mwaka huu, Edday alimwandikia Samidoh ujumbe mrefu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimuonya kwamba hayuko tayari kamwe kulea watoto wao katika ndoa ya wake wengi.