logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ndoa 2 kwa kila ndoa 3 nchini zimeshuhudia visa vya kucheat mwaka mmoja uliopoita - ripoti

Ndoa 2 kwa kila ndoa 3 nchini zimeshuhudia kisa cha kucheat kwa mwaka mmoja ulipoita.

image
na Davis Ojiambo

Burudani17 July 2023 - 09:37

Muhtasari


  • • Utafiti uliofanywa na kampuni ya Research and Insigts Group umefichua kuwa angalau ndoa mbili kwa kila ndoa tatu nchini zimeshuhudia kisa cha udanganyifu.
  • • Kwa upande mwingine asilimia 65 ya wanaume nchini walikiri kuwa na uhusiano nje ya ndoa.

Utafiti uliofanywa na kampuni ya Research and Insigts Group umefichua kuwa angalau ndoa mbili kwa kila ndoa tatu nchini zimeshuhudia kisa cha udanganyifu ndani ya mwaka moja uliopita.

Kulingana na ripoti hiyo, ndoa nyingi nchini zimeshuhudi zisa vya usaliti katika mahusiano ya kimapenzi huku asilimia 35 ya wanawake wakikiri kuwa na mahusiano nje ya ndoa angalau mara moja.

“Angalau mbili katika kila ndoa 3 nchini kenya, kumekuwa na visa vya udanganyifu katika mwaka uliopita. Zaidi ya hayo asilimia 35 ya wanawake walioolewa walikiri kuhusika katika uhiano nje ya ndoa mara moja.”

Utafiti huo huo ulifichua kuwa kati ya wanawake 3 waliohusika katika utafiti huo, mwanamke mmoja kati ya watatu walikiri kuhusika kwenye mapenzi ya usiku mmoja na mwanaume wasiokuwa na uhusiano wowote baina yao.

Kwa upande mwingine asilimia 65 ya wanaume nchini walikiri kuwa na uhusiano nje ya ndoa huku wanaume asilimia 73 wakiongeza kuwa ikiwa wangeshikwa wakicheat bado wangerudi kutafuta mahusiano nje ya ndoa.

Asilimia 20 ya wanawake walisema kuwa ikiwa wangekamatwa na bwana zao kwenye uhusiano nje ya ndoa wangerudi kwenye soko na kucheat bado ikilinganishwa na asilimia 73.

Visa vya wanawake kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume wenye umri mdogo kuwashinda vimekuwa vikiongezeka huku wanawake wachanga wakilalalimika kuibiwa wapenzi na wanawake wazee wenye hela.

Utafiti huo ulibainisha hili kuwa kweli kwani asilimia 30 ya wanawake nchini walikiri kushiriki mapenzi na wanaume wadogo kiumri kwao almaarufu Ben 10. Wanawake hawa waliwachukulia vijana kuwa wenye nguvu na kuwatosheleza kingono.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved