In Summary

•Vera alionyesha video yake na mwanamume asiyejulikana wakiwa kwenye gari wakielekea kwenye eneo la burudani katika jiji la New York.

•Haya yalitokea saa chache  baada ya Brown Mauzo kudokeza kuwa yuko tayari kuendelea na hatua inayofuata baada ya uhusiano wao kuvunjika.

Vera Sidika amevunja kimya baada ya Brown Mauzo kutangaza wameachana.
Image: INSTAGRAM

Mwanasholaiti maarufu Vera Sidika amewaacha wanamitandao wa Kenya wakizungumza baada ya kudokeza kuwa huenda tayari amezama kwenye mahusiano mengine, siku chache tu baada ya kutengana kwake na mwimbaji Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo kujulikana hadharani.

Siku ya Alhamisi, mama huyo wa watoto wawili ambaye kwa sasa anafurahia likizo yake ya msimu wa joto  nchini Marekani alionyesha video yake na mwanamume asiyejulikana wakiwa kwenye gari wakielekea kwenye eneo la burudani katika jiji la New York.

Kilichovuta hisia za wengi ni jinsi mwanasosholaiti huyo na mwanaume huyo ambaye mkono wake pekee ulionekana walivyoshikana kimahaba. Wawili hao walishikana mikono kwa karibu huku wakifurahia muziki wa kimahaba uliokuwa ukipigwa ndani ya gari.

Baadaye Vera alishiriki video zaidi zilizomuonyesha akifurahia wakati katika eneo la burudani.

Haya yalitokea saa chache tu baada ya mzazi mwenzake, Brown Mauzo kudokeza kuwa yuko tayari kuendelea na hatua inayofuata baada ya uhusiano wao kuvunjika.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Siku ya Jumatano, mwimbaji huyo alitangaza kwamba anatafuta rafiki ambaye anaweza kufurahia wakati kitandani naye.

"Nataka rafiki bora nitakayelala naye," alisema.

Wiki iliyopita, mwanamuziki Brown Mauzo alitangaza kuwa wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Mauzo aliendelea kumshukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Mauzo alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhsu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.

View Comments