logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mrembo ashangilia kutarajia mtoto mwingine miezi 2 baada ya kuzaa, aonyesha kitumbo (Video)

Kwa tathmini ya haraka, kitumbo hicho kinaonekana kama ya miezi Zaidi ya mitano .

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 January 2024 - 09:17

Muhtasari


  • β€’ Anaonekana akicheza sana kama njia ya kueleza furaha yake kubwa ya kumkaribisha mtoto mpya hivi karibuni ingawa alimkaribisha mtoto miezi 2 iliyopita.
Mwanamke mwenye mimba n mtoto wa miezi 2

Mwanamke mmoja aliye na mtoto mkono amewashangaza wengi baada ya kudai kwamba tena ana ujauzito, miezi miwili tu baada ya kujifungua mtoto wa kwanza.

Katika video mpya ambayo imezua utashi katika mitandao ya kijamii, mrembo huyo ambaye mkononi amepakata mtoto wa miezi miwili anaonekana akiruka kwa furaha huku kitumbo cha mimba kikiwa wazi.

Kwa tathmini ya haraka, kitumbo hicho kinaonekana kama ya miezi Zaidi ya mitano na hivyo taswira nzima iliwaacha wengi katika hali ya kuchanganyikiwa ikiwa kweli alikuwa anasema ukweli.

Mwenyewe aliandika katika video hiyo kwamba mumewe alimpa mimba miezi wakati tayari ana mtoto wa miezi miwili mkononi.

Anaonekana akicheza sana kama njia ya kueleza furaha yake kubwa ya kumkaribisha mtoto mpya hivi karibuni ingawa alimkaribisha mtoto miezi 2 iliyopita.

Akinukuu video hiyo, mwanadada huyo aliandika; “Mume wangu alinitwanga mimba nyingine na mtoto wangu wa miezi miwili.”

Hata hivyo baadhi walitofautiana naye wakisema kwamba haiwezekani mama mwenye mtoto wa miezi miwili awe na mimba kubwa kama hiyo ambayo inakaa ni ya miezi Zaidi ya mitano.

“Huyo ndio tu tumbo lake linatokea nje baada ya kujifungua, ni muongo hana mimba,” effedeborah alisema.

“Kwa kweli mitandao ya kijamii imefanya mengi mabaya kuliko mazuri,” mwingine alisema.

“Huyo mtoto anaweza hata asiwe wake …..Mimba yake ni hadi miezi 6/7 na ukiangalia mtoto huyo ana umri wa miezi 3 hesabu yote haingiani,” Ruthemily alisema.

“Eti mtoto wa miezi miwili na ukubwa wa mimba yote hii? Toka hapa wewe nenda ukamlee mtoto,” mwingine alimkaripia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved