Mwanamke mfanyabiashara asiye na mume mwenye umri wa miaka 38 kutoka amejitokeza kwenye mitandao ya kijamii kutangaza nia yake ya kutoa shilingi milioni 50 kwa mwanamume yeyote atakayekubali kumuoa.
Inaarifiwa kwamba Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Ella Ada, ni mmiliki wa shamba kubwa la kuku na anatafuta mume ambaye hangehitaji kuhangaikia majukumu ya kifedha.
Video iliyotumwa na mtumiaji wa TikTok @signedollar inamuonyesha mwanamke huyo akiwa ameshika bango linalosomeka: “Nahitaji mume. milioni 50 kwa yeyote atakayenioa.”
Katika video hiyo, anaeleza waziwazi tamaa yake ya kuwa na mwanamume mtiifu ambaye atakuwa tayari kumuoa na kufurahia maisha ya starehe bila wasiwasi wa kifedha.
”Kuwa tu mume mtiifu. Ninachohitaji ni mtu anayejali sana, mtiifu. Usijisumbue kuhusu harusi; Mimi ndiye nitakayeifadhili. Sitaki mume wangu ateseke hata kidogo…” alisema kwa sehemu.
Pendekezo la Ella Ada limezua wimbi la mijadala mtandaoni, huku wengi wakieleza maoni yao.
Licha ya kuweka wazi kwamba atamlipa mwanamume atakayemuoa, wengi walishangazwa na yeye kusisitiza kigezo cha mwanamume mtiifu, wakisema kwamba hakuna mwnamume atakayeuza utu wake kwa 50m ili kwenda kuwa chini ya mwanamke.
@talentedcreative01 alisema: "Ni kama ulikuwa na uhaba wa wafanyakazi na kumtafuta mmoja atakayekuwa wa kudumu."
@michaelezeh11 alisema: “Bibi nina biashara yangu mwenyewe. Utakuwa mama yangu wa nyumbani, utunze watoto wangu, na unipikie.”
@Miles USDT FC alisema: "Nahitaji mwanamke wa kuoa sio mwanamke wa kunioa."
@MJ alisema: "Naipenda hii ..Mungu akupe hitaji la moyo wako Nne."
@kpoi functional alisema: "Nenda kwenye kituo cha redio na ukitangaze kwamba unahitaji mfanyakazi wa nyumbani."
Tazama hapa chini;