logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mama alidanganya!" Tiffah apigwa na butwaa baada ya Diamond kumfanyia surprise ya kupendeza

Diamond alim’surprise bintiye Latiffah kwa kujitokeza kwenye sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa bila yeye kujua.

image
na Samuel Maina

Burudani11 August 2024 - 08:10

Muhtasari


  • •Diamond alim’surprise bintiye Latiffah kwa kujitokeza kwenye sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa bila yeye kujua.
  • •Tiffah alionekana kupigwa na butwaa akimkaribisha babake kwenye tafrija hiyo ya kifahari iliyohudhuriwa na familia na marafiki.
wakati wa sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya Tiffah

Staa wa Bongo Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz alim’surprise bintiye Latiffah Dangote kwa kujitokeza kwenye sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa bila yeye kujua.

Diamond aliwasili nchini Afrika Kusini siku ya Jumamosi, akiwa ameandamana na timu yake na wakaenda mpaka mahali palipokuwa pakifanyika sherehe ya bintiye. Baada ya kuwasili, alibainisha kuwa alikuwa na nia ya kum’surprise mtoto huyo wake wa kwanza kwani hakuwa na taarifa kwamba angehudhuria sherehe hiyo.

Mwimbaji huyo alikaribishwa na jamaa na marafiki wa mzazi mwenzake Zari. Tiffah ambaye alikuwa hajui kinachoendelea alikuwa akicheza na marafiki zake wakati baba yake alingia chumbani.

Nilidhani hutakuja. Mama alisema hautakuja. Mama alidanganya,” Tiffah alisema huku baba yake akimnyanyua juu.

Malkia huyo mdogo ambaye hivi majuzi alifikisha umri wa miaka tisa alionekana kupigwa na butwaa alipokuwa akimkaribisha babake kwenye tafrija hiyo ya kifahari iliyohudhuriwa na familia na marafiki zake.

Video nyingine za tukio hilo zilimuonyesha Diamond akiimba wimbo wake maarufu ‘Komasava’ pamoja na watoto wake, akiwakabidhi zawadi na kutengeneza kumbukumbu nyingine nzuri nao. Mwimbaji wa WCB, D-Voice ambaye alikuwa ameambatana na bosi wake kwenye hafla hiyo pia alionekana akiwaburudisha wageni wakati tafrija ikiendelea.

Diamond alikuwa amebeba vitu vingi vya kuchezea pamoja na zawadi nyingine kwa ajili ya kuwasherehekea bintiye na mtoto wake wa kiume Prince Nillan, na walionekana kuzifungua kwa furaha.

Tiffah, ambaye ni binti wa staa huyo wa bongo fleva na sosholaiti kutoka Uganda Zari Hassan aligonga umri wa miaka 9 mnamo Agosti 6.

Zari alimsherehekea bintiye kwa kuchapisha picha zao nzuri wakiwa pamoja. Alimtaja msichana huyo wa miaka 9 kuwa ni Malkia wa Tanzania.

"Nisaidie kumtakia binti yangu wa pekee, Malkia wa Tanzania, siku njema ya kuzaliwa @princess_tiffah👗@hers_uganda," aliandika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved