logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bradley apata mpinzani, Isaac Otesa anadai kuwa mrefu zaidi

Isaac Otesa amejitokeza na kudai kuwa mrefu zaidi kuliko Bradley aka Gen Z Goliath.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 August 2024 - 12:52

Muhtasari


  • •Isaac Otesa anasema ya kuwa yeye ni mrefu kumliko Bradley Marongo ambaye anajulikana kama 'Bradley Mtall'. Ili kuthibitisha anataka kukutana naye.
Bradley,Isaac

Huenda kukawa na ushindani baina ya jamaa wawili Bradley Marongo na Isaac Otesa huku kila mmoja akidai kuwa mrefu kuliko mwingine.

Kwa wiki chache ambazo zimepita, Bradley ambaye anajulikana kama 'Gen Z Goliath' amepata umaarufu mtandaoni kutokana na urefu na ukubwa wake. Hata hivyo, Bradley hajapata kufurahia umaarufu wake kwa muda mrefu kabla ya Isaac Otesa kujitokeza na kudai kumshinda urefu.

 Kwa video Isaac anasema kuwa yeye ni mrefu wa Bradley kwani yeye ana urefu wa futi 8.4 mwenzake akiwa na urefu wa futi 8.2. Anaomba kukutana na Bradley ili kuthibitisha ni nani mrefu kati yao wawili."yeye ni mfupi mimi ni mrefu...mimi natamani nifike mahali ako nione urefu wake kama ananishinda ama hanishindi"

Picha zaonyesha kufanana kati ya jitu hao wawili ila Bradley anatoka kaunti ya Vihiga na Isaac anatoka kaunti ya Bungoma. 

Je, ni wazo nzuri kuwa na mashindano kati ya hao jitu wawiwli?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved