Huddah Monroe amekiri kuwa yuko tayari kuwa katika ndoa ya wake wengi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Huddah alisema kuwa atamruhusu mumewe mtarajiwa kuoa mke wa pili.
Mwanasosholaiti hata hivyo alidokeza kuwa ni sharti mwanaume awe na pesa za kutosha kabla ya kuoa mke mwingine.
'Sijali mume wangu kuoa mke wa pili ikiwa ni tajiri na anaweza kututunza, kwa sababu sifikirii kumhudumia mume wangu kwa maisha yangu yote,'' Huddah alisema.
Kwa kawaida, mwanasoshalaiti huyo huwa haogopi kusema anachofikiria au kutangaza matamanio yake.
Monroe huwa hajali maoni ya watu kuhusu kile anachochapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Huku hayo yakisemwa, Huddah huwafahamisha wafuasi wake kuhusu kile anachofikiria kuhusu maisha yake.Siku za hivi majuzi amekuwa akiangazia masuala ya ndoa.
''Wakati fulani nitakuwa nimechoka, na atakuwa mzee pia, kila mmoja anachoka kadri muda unaposonga'' Huddah alisema.
Kwa sasa hakuna yule ambaye ana ukweli wa mambo kuhusu mahusiano ya mwanasosholaiti huyo.
Inadaiwa kuwa yupo kwenye mahusiano na mkali wa muziki wa RnB kutoka Bongo, Juma Musa Mkambala almaarufu Juma Jux .
Lakini Jux aliweka wazi kuwa yeye na Huddah ni marafiki tu na hakuna uhusiano yoyote kati yao.
Huddah ambaye sasa amefikisha mwaka thelathini anajifurai maisha yake ya ukapera akijipa moyo kuwa kuna siku naye pia ataolewa na kufurahia ndoa yake.