In Summary

•Obinna alimtaka mchekeshaji huyo kujibu madai kwamba alitelekeza majukumu ya anayedaiwa kuwa mtoto wake na Jackie Maribe.

•Obinna alimbainishia Eric kuwa mtoto ambaye walikuwa wakizungumzia anafanana naye kama shilingi kwa ya pili.

Eric Omondi na Jacque Maribe

Mchekeshaji Eric Omondi alilazimika kujibu madai ya kuwa baba asiyewajibika wakati wa mahojiano ya wazi na mtangazaji Oga Obinna.

Katika mahojiano hayo, Obinna alimtaka mchekeshaji huyo kujibu madai kwamba alitelekeza majukumu ya anayedaiwa kuwa mtoto wake na Jackie Maribe.

Eric hata hivyo alionekana kukwepa kujibu swali hilo moja kwa moja akisema kuwa hayuko huru kuzungumzia suala hilo kwani anahofia kufikishwa mahakamani.

“Watoto ni baraka iwe ni wako au  la. Mtoto akishajua kuwa wewe ni baba yake, jambo bora zaidi unaweza kufanya ni kumlea kama baba yake,” Eric Omondi alisema kwa kujipendekeza.

Kufuatia jibu la kimafumbo la mchekeshaji huyo, Obinna alimshauri kwamba kuna chaguo la wazazi kufanya DNA na kumbainishia kuwa mtoto ambaye walikuwa wakizungumzia anafanana naye kama shilingi kwa ya pili.

Mapema mwaka jana, Eric Omondi alisema kuwa hakuna uhasama wowote kati yake na Jacque Maribe ambaye anadaiwa kuwa mzazi mwenzake.

Katika mahojiano na Mpasho, Omondi alisema kwa sasa uhusiano wake na Bi Maribe ni mzuri kufuatia mazungumzo mazuri ambayo walishiriki 2021.

Omondi ambaye anaaminika kuwa baba ya mtoto wa mtangazaji huyo alisema ingawa hawakurejesha mahusiano ya kimapenzi, wao ni marafiki.

"Tulikutana, tukazungumza na kukubaliana. Kwa sasa sisi ni marafiki. Tuko sawa mimi na Jacque" Eric alisema.

Mchekeshaji huyo hata hivyo aliweka wazi kwamba hatakuwa anaonyesha uhusiano wake na mzazi huyo mwenza hadharani.

Mwaka wa 2021, wasanii hao wawili ambao walidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi katika miaka ya nyuma walivuana nguo hadharani na kutupiana cheche za maneno kuhusiana na majukumu ya malezi.

Ugomvi wao ulikuwa mbaya kiasi cha Eric kufikia hatua ya kuibua shaka ya kuwa mzazi mwenza wa mtangazaji huyo wa zamani wa habari. Huku wakiendelea kujibizana, wakati mmoja alidai kwamba alishiriki tendo la ndoa na Maribe mara moja tu mnamo mwaka wa 2012 baada ya wao kubugia chupa kadhaa za mvinyo. 

"Tulipatana Radio Africa mwaka wa 2012. Nilikuwa nafanya kazi Radio Jambo na Jacque alikuwa anafanya kazi Kiss TV. Usiku mmoja baada ya sherehe na kunywa chupa kadhaa za whiskey na mvinyo Jacque na mimi ikatendeka. Ilikuwa jambo la usiku mmoja kwani alikuwa anachumbia Sam Ogina wa KTN" Omondi alisema. 

Mchekeshaji huyo asiyepungukiwa na drama alidai kwamba alihakikisha kwamba ametumia kinga wakati aliposhiriki mapenzi na Maribe.

Wawili hao baadaye walipatanishwa na mfanyibiashara Simon Kabu na hatimaye wakaomba radhi kwa Wakenya kwa waliyosema hadharani.

View Comments