In Summary

•Akothee alifunguka jinsi alivyogundua mtindo wa babake wa kupumua usio wa kawaida, jambo liliopelekea ziara hiyo ya hospitalini.

•Akothee alizungumzia jinsi Bw. Kokeyo hapendi kupelekwa hospitalini kuchunguzwa na jinsi huwa anapinga.

Akothee na baba yake Joshua Kokeyo
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Siku ya Jumanne, mwanamuziki Esther Akoth almaarufu Akothee alichapisha video iliyomuonyesha akimpeleka hospitalini baba yake Joshua Owino Kokeyo ili kuchunguzwa.

Kwenye maelezo ya video hiyo, mwimbaji huyo alifunguka kuhusu jinsi alivyogundua mtindo wa babake wa kupumua usio wa kawaida, jambo liliopelekea ziara hiyo ya hospitalini.

Alizungumzia jinsi Bw. Kokeyo hapendi kupelekwa hospitalini kuchunguzwa na jinsi huwa anapinga. Hata hivyo, aliamua kumpeleka kuangaliwa kwani mtindo wake wa kupumua usio wa kawaida ulimfanya awe na wasiwasi sana usiku kucha.

“Thubutu kumwambia Baba yangu ni Mgonjwa utajua. Wakati wowote unapofika wa kumpeleka kwa uchunguzi, atakuuliza, “Unasema mimi ni mgonjwa, ninaumwa na nini? Ninaonekana mgonjwa kwako?" Akothee alisema chini ya video aliyoshiriki kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Aliongeza, "Lakini leo sikupenda mtindo wake wa kupumua, niligundua kuwa hakuweza kuimba, Hii ilinisumbua Usiku Wote. Kutoka kokote aliniambia anammiss mama yake na anatamani kuona picha ya mama yake.”

Mama huyo wa watoto watano alidokeza kuhusu upendo wake mkubwa kwa mzazi huyo wake na akamuomba Mungu amjalie afya njema.

Babake Akothee, Bw Joshua Owino Kokeyo ni afisa wa zamani wa Wilaya na kwa sasa anaishi nyumbani kwao katika kaunti ya Migori.

Takriban mwaka mmoja uliopita,  Akothee ​​ alifunguka kuhusu ugonjwa wa mzazi huyo wake ambao ulimfanya ashindwe kuhudhuria shoo zake.

''Mshauri wangu siwezi kuanza kuandika chochote, ninachojua ni kwamba wewe huji tena kwenye hafla zangu. Nimelia sana, na bado sikatii tamaa'' ' Akothee alisema mnamo siku ya kuwaadhimisha kina baba mwaka jana.

Mwanamuziki huyo alifunguka kuhusu jinsi  wakati mwingine alivyokosa ujasiri wa kuzungumza naye kwa sababu ya hali yake.

''Sizungumzi na wewe mara nyingi kama hapo awali kwa sababu nimeachwa nikijiuliza maswali mengi,'' Akothee alisema.

Alisema kuwa kudhoofka kwa afya ya babake ni jambo ambalo ameshindwa kuishi nalo, na hayuko  tayari kukubali hatima hiyo.

''Siamini jinsi ulivyo sasa hivi, haya si maisha ambayo ulikua umezoea kuishi '' Akothee alisema.

Mfanyibiashara huyo pia alifichua  kuwa mawasiliano kati yake na baba yake kupitia simu yamekuwa finyu.

''Hatuongei kwa njia ya simu kama tulivyokuwa tunazungumza baba, sikutumii pesa, kwa sababu ukishakuwa na pesa unasahau mahali unapoweka pesa yako''Akothe alisema.

Wakati huo, Akothee alidai kuwa hajui  ikiwa anapaswa kuendelea kuhifadhi  nambari ya simu ya babake  kwenye simu  yake ya mkono au kuifuta.

''Mungu akuponye baba nakupenda na naninakukosa sana moyoni',' alisema.

View Comments