In Summary

•Lilian Nganga ambaye ni mama wa mtoto mmoja  alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 38 kwa njia ya kipekee.

•"Siku yangu ya kuzaliwa ni Aprili 22, Mpenzi wangu Juni 22, alafu mtoto wetu Julai 22.. 2 much," Juliani alifichua

Lilian Nganga na mume wake Juliani
Image: INSTAGRAM// JULIANI

Mkewe mwimbaji Juliani, Bi Lilian Nganga aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mnamo Alhamisi, Juni 22.

Lilian ambaye ni mama wa mtoto mmoja  alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 38 kwa njia ya kipekee na alishiriki baadhi ya maelezo ya sherehe hizo kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Kwenye Instagram, alionyesha video ya keki nzuri na maua ambayo yalikuwa sehemu ya karamu yake ya Alhamisi jioni.

"Birthdays.. 38," aliandika.

Rapa Juliani ambaye kwa jina halisi ni Julius Owino  alitumia siku hiyo kutangaza upendo wake mkubwa kwa mama huyo wa mwanawe, Utheri.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, alimmiminia Lilian maneno matamu na kumtaja kwa majina mazuri huku akimtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

"Nyar Okuyu.

Msichana switi, peremende.

Gal sambaratisha my heart.

Miss mwah! Mwah!

Mtoto fine thank you. 

Happy birthday , Mpenzi," Juliani aliandika.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha nzuri iliyomuonyesha akiwa amesimama pamoja na mpenzi huyo wa zamani wa waziri Alfred Mutua.

Katika chapiho lingine, mwanamuziki huyo alifichua  maelezo maalum kuhusu siku ya kuzaliwa ya mkewe, mtoto wao na yeye mwenyewe.

"Siku yangu ya kuzaliwa ni Aprili 22, Mpenzi wangu Juni 22, alafu mtoto wetu Julai 22.. 2 much," Juliani alifichua

Mwimbaji huyo na mkewe Lilian Nganga walimkaribisha mtoto wao wa kwanza pamoja duniani, Utheri, mnamo mwezi Julai mwaka jana, takriban mwaka mmoja tu baada ya kuyaweka wazi mahusiano yao.

Akizungumzia jinsi ulezi wa Utheri umekuwa mnamo mwezi Machi, mke huyo wa zamani wa waziri wa Masuala ya Kigeni Alfred Mutua alibainisha kuwa imefufua baadhi ya mambo ya kitoto aliyofanya miaka ya nyuma.

"Kulea mtoto huyu kumeamsha utoto ulio ndani yangu ambao ulikuwa umesahaulika kwa muda mrefu," Bi Nganga alisema.

Mama huyo wa mvulana mmoja aliweka wazi kuwa anafurahia sana hatua ya kumlea mwanawe na mambo ambayo imemlazimu kufanya.

"Ninaipenda kwa ajili yangu.. kwa ajili yake.. kwa ajili yetu," alisema.

Juliani alifichua kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza na mkewe Lilian Nganga akiwa kwenye mahojiano mapema mwezi Agosti.

Akizungumza na Presenter Ali, mwimbaji huyo wa nyimbo za kufoka alitangaza habari kwamba walipokea zawadi ya mtoto wa kiume siku zilizokuwa zimepita na kuweka wazi jinsi alivyofurahi kuwa baba tena.

 "Nina watoto wawili. Msichana na mvulana. Nilimkaribisha mtoto wa kiume hivi majuzi na Lilian Ng'ang'a," alisema.

Juliani na Lilian walifunga ndoa katika Paradise Lost mnamo Februari 2, 2022, mbele ya familia na marafiki wa karibu.

Orodha ya wageni ilikuwa chini ya watu 50. Ilikuwa wakati huo ambapo Wakenya waligundua Lilian alikuwa anatarajia mtoto.

View Comments