In Summary

•Mama Dangote aliweka picha za kumbukumbu za  Diamond akiwa mtoto na kumfananisha na mtoto wake mdogo wa kiume, Naseeb Jr.

•Kwa chapisho hilo, mamake Diamond alionekana kumuidhinisha mtoto wa Tanasha Donna kama mteule kati ya wajukuu zake.

Image: INSTAGRAM// MAMA DANGOTE

Mama ya mwimbaji wa bongo Diamond Platnumz, Bi Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote kwa mara nyingine ameonyesha wazi kuwa mtoto wa Tanasha Donna na mwanawe, Naseeb Junior ndiye mjukuu wake kipenzi.

Siku ya Jumatano, aliweka picha za kumbukumbu za bosi huyo wa WCB alizopigwa akiwa mtoto na kumfananisha na mtoto wake mdogo wa kiume, Naseeb Jr.

Mama Dangote pia alionekana kubainisha kwamba mvulana huyo wa miaka minne ndiye toleo ndogo la kweli la staa huyo wa bongo fleva.

"Huyu ndiye @diamondplatnumz!" Mama Dangote alisema.

Kwa chapisho hilo, mamake Diamond Platnumz alionekana kumuidhinisha mtoto wa Tanasha Donna kama mteule kati ya wajukuu zake.

Aidha, alishiriki picha zaidi za kumbukumbu za Diamond akiwa mtoto na kuzilinganisha na zile za Naseeb Jr kuonyesha jinsi wanavyofanana.

Sio mara ya kwanza kwa Mama Dangote kuonyesha waziwazi kuwa anampendelea mwana huyo wa mwisho wa Diamond zaidi ya watoto wake wengine. Mwishoni mwa mwaka jana, aliweka wazi kuwa Naseeb ndiye rasmi mrithi wa Diamond Platnumz katika biashara ya Wasafi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mama Dangote alipakia picha ya Diamond akiwa na mwanawe huyo na kusema kuwa rasmi amemkabidhi kijiti cha kuwa mrithi wa mwanawe Simba, Diamond Platnumz.

Mr. Tom kaka mdogo leo namkabidhi kijiti cha wasafi 👬Mimi mwenyewe,” Mama Dangote alitangaza bayana.

Wengi walifurahishwa na mfanano ulioko kati ya Diamond na mwanawe huku wakisema kuwa uzuri wa baba umeonekana wazi kwenye panda la uso la mwanawe.

View Comments