logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Erick Omondi amenizimia data, hachukui simu zangu - Miss P.

Msanii wa kike Miss P amesema kwamba mcheshi Erick Omondi alikwenda kimya baada ya kazi mbili za muziki alizomsaidia kuachilia.

image
na

Habari02 February 2022 - 11:14

Muhtasari


• Msanii wa kike Miss P amesema kwamba mcheshi Erick Omondi alikwenda kimya baada ya kazi mbili za muziki alizomsaidia kuachilia.

• Ametaja kwamba anamshukuru Omondi kwa kuasisi mchakato wa kuwez kumrudisha kwenye game, akisema kwamba milango mingi imefunguka na amepiga hatua kubwa tangu kipindi hicho.

Miss P

Msanii wa kike Miss P amesema kwamba mcheshi Erick Omondi alikwenda kimya baada ya kazi mbili za muziki alizomsaidia kuachilia.

Ametaja kwamba anamshukuru Omondi kwa kuasisi mchakato wa kuwez kumrudisha kwenye game, akisema kwamba milango mingi imefunguka na amepiga hatua kubwa tangu kipindi hicho.

Miss P amekiri kwamba aliamua kuendelea kujisukuma ili kukuza jina lake zaidi kwenye burudani la Kenya, licha ya Omondi kutoonyesha dalili yoyoyte ya kuendelea kumsaidia kukuza kipaji chake.

Aidha amesisitiza kwamba hawezi kamwe kurudi kufanya  kazi yoyote na msanii Willy Paul, ikifahamika kwamba Miss P alikuwa chini ya Saldido Record ila baadaye wakaibuka kutengana kwa misingi ya Willy Paul kujaribu kumtumia kimapenzi.

Mwanamuziki huyo amesema kwamba kuna ngoma moja ambayo alifanya na Willy Paul na haikufanikiwa kudondoshwa na angependa sana kurudi ili waachilie kazi hiyo , kwa kuwa   ni ngoma ambayo aliipenda sana na hiyo ndio pekee inaweza kumfanya wazungumze naye halafu basi tu.

Miss P ambaye hayupo chini ya usimamizi wowote kwa sasa, amewahakikishia mashabiki wake kwamba atazidi kutoa kazi za kuburudisha.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved