logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KRG the Don anasema mahari inafaa kurudishwa baada ya kuachana

Msanii wa Gengetone KRG the Don anahoji ni vema mahari kurudishwa baada ya wapenzi kuachana.

image
na Davis Ojiambo

Burudani02 February 2022 - 09:27

Muhtasari


  • • Msanii wa Gengetone KRG the Don anadai ni vema mahari kurudishiwa baada ya wapenzi wawili kuachana.
  • • KRG the Don anadai kwamba, ni vizuri mahari kurudishiwa familia ya mwanaume baada ya watu kuachana ili ikutolee nuksi katika mahusiano yako yanayofuata.

Msanii wa Gengetone KRG the Don anadai ni vizuri mahari kurejeshewa wenyewe baada ya kukosekaan kwa maelewano baina ya wapenzi katika ndooa, kama hili litasababisha kuachana.

KRG the Don anadai kwamba, ni vizuri mahari kurudishiwa familia ya mwanamume baada ya watu kuachana ili ikutolee nuksi katika uhusiano wako ujao.

“Watu mkishaachana, ni jambo la busara kurudisha vitu vya watu kwa sababu huyo mwanamume labda hiyo ndio ilikuwa mali yake ya mwisho na ataitumia kuchukua mwanamke mwingine. Kwa hiyo ni vizuri kurudishia mwanaume vitu vyake ili aendelee na Maisha yake,” alisema KRG katika mahojiano kwenye blogu ya SPM Buzz kwenye mtandao wa YouTube.

Baba huyo wa Watoto wawili anasikika katika mahojiano hayo akiteta vikali kwamba wawili waliopendana wakisha achana, mahari inarudishwa ili kufungulia mwanamke huyo baraka katika kuolewa kwingine tena.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved