logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Unakosa pesa ya kitunguu anakuanika mitandaoni kuwa umesota" Mustafa azungumza kuachana na Noti Flow

"Unakuwa na mke au mchumba umekosa kitunguu anaenda mitandaoni anapakia “amekosa pesa ya kitunguu huyu amesota” - Colonel Mustafa.

image
na Radio Jambo

Habari07 July 2022 - 12:34

Muhtasari


• Colonel Mustafa alisema alijifunza na hawezi ingia mahusiano na mtu wa mitandaoni.

Msanii mkongwe wa Kenya

Msanii mkongwe wag emu la muziki nchini Kenya Colonel Mustafa amefunguka ya ndani kile kilichomfanya kuvunja mahusiano yake na mwanamama Noti Flow, ambaye kwa sasa ni shoga.

Mustafa kipindi cha miaka ya nyuma walikuwa katika mahusiano ya Noti Flow ambaye pia ni msanii na mapenzi yao yalikuwa ni hadithi nzuri ya kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii haswa kutokana na sababu kwamba hawakuwa wanaficha kitu – walikuwa wanaweka wazi kweney mitandao ya kijamii.

Staa huyo aliyetamba na kibao ya Monalisa alielezea kwamba aliamua kuchukua likizo ndefu ya mapenzi baada ya kuachana na Noti Flow kwani mahusiano yake licha ya wengi mitandaoni kuyaona kama mfano wa kuiga lakini nyuma ya kamera yalikuwa ni mfano wa onyo kwa wengi.

Alionekana kudokeza kwamba Noti Flow alikuwa anampa shinikizo la aina fulani baya tu bila kujua kwamba wakati mwingine mwakaume hana uwezo wa kikidhi mahitaji ya kila kitu kwa muda ule unaohitajika.

“Niliona nitulie tu. Niliona hakuna haja tena mimi kuingia kwenye mahusiano kwanza ya kujionesha sana, nadhani nilishajifunza hayasaidii kwa sababu haileti maana unakuwa na mke au mchumba umekosa kitunguu anaenda mitandaoni anapakia “amekosa pesa ya kitunguu huyu amesota” na unakuwa hautulii tena uko chini ya shinikizo, kwa hiyo niliona bora nitulie nikuwe vna mtu mwenye hayuko kwenye media, mtu anafanya shughuli zake,” alifunguka ya moyoni Colonel Mustafa.

Msanii huyo mkongwe pia alifichua kwamab kuna muda ilibidi atoke kidogo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kile alikitaja kuwa unyongovu ulizidi ambapo kila mtu alikuwa anataka kumtumia vibaya akaona ni heri ajitoe tu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved