logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Zuchu amfuata Diamond Ufaransa "Mapenzi Ulaya"

Zuchu amepakia video akionekana na Diamond huko Ufaransa ambapo msanii huyo yuko katika ziara ya kuiuza albamu yake ya FOA

image
na Radio Jambo

Yanayojiri23 July 2022 - 12:00

Muhtasari


• Katika video ambazo Zuchu na mamake Diamond walipakia kwenye instgram zao, Zuchu anaonekana akijumuika na Diamond huko Ufaransa.

Mambo ni mengi saa ndio chache!

Unaambiwa kwamba msanii Diamond ambaye yuko ziarani katika bara Uropa tangu wiki jana alipotumbuiza kwenye tamasha la Afro Nations lililofanyika nchini Ureno na kisha baadae kuelekea nchini Ujerumani ambapo alitumbuiza kwenye tafrija mbalimbali zilizosheheni ushabiki wa ajabu, sasa msanii mwenza kutoka lebo yake ya Wasafi, Zuchu amemfuata kule kule Ulaya.

Katika video ambazo Zuchu alipakia kwenye instastories zake pamoja na Sandra, mamake Diamond, Zuchu anaonekana kujumuika na msanii Diamond nchini Ufaransa ambapo Simba anaendeleza mbinginyo wa gurudumu la kusukuma muziki wake ili kufahamika zaidi nje ya bara la Afrika.

Wiki juzi wakati Diamond alikuwa bado ziarani huko Ulaya, ilisemekana kwamab Zuchu alikuwa nchini Afrika Kusini kushughulikia video za ngoma zake mpya, jambo lililomfanya mwanadada huyo kukosa kuhudhuria sherehe za siku ya kuzaliwa ya Mama Dangote.

 Sasa haijulikani Zuchu kamfuata Diamond Ulaya kwa ajili ya kazi ama kujivinjari tu pamoja na wawili hao hakuna aliyesema kitu chochote mpaka sasa.

Diamond na Zuchu kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakisemekana kwamba wako katika mahusiano ya kimapenzi ila bado haijawahi wekwa wazi na upande wowote kudhibitisha wala kupuuza madai hayo, ila kwa mara nyingi tu wamekuwa wakionekana pamoja katika njia yenye ukakasi mkubwa mpaka kuwafanya wengi kuamini kwamba huenda Diamond anamvizia malkia huyo wa Bongo Fleva.

Wiki jana katika moja ya mahojiano ya moja kwa moja na vyombo vya habari nchini Ujerumani alisema kwamba yeye hana mpango wowote wa kuingia katika ndoa hivi karibuni na kusema kwamab aliamua kufanya uamuzi huo kwa saababu alikuwa anataka kuwapa mashabiki wake muziki.

Diamond alisema kwamab kwa sasa ni muziki tu anataka kufanya na hataki kuuchanganya kabisa na mambo ya ndoa au wanawake kwani katika kile alichokitaja kwamba ameona kwa rafiki zake, pindi mwanamuziki anaingia katika mahusiano na mwanamke basi anafifia na kudidimia kabisa kimuziki.

Aidha, alisema kwamab hawezi kamwe kulifutilia mbali suala ka kuoa kwani atafanya maamuzi hayo wakati anakaribia kustaafu.

Ila swali sasa ni je, Zuchu alimfuata Ufaransa ama kila mtu alienda huko kwa hamsini zake kabla ya kukutana ghafla? Je ni Diamond aliyemuita kumpa kampano huko Ulaya?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved