logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Ukitaka kufa mapema, changanya umaskini na wivu, ongeza Ushindani!" - Aunty Ezekiel

“Ukitaka kufa mapema tu Changanya umaskini na wivu basi ongeza Ushindani, niamini mimi, hata madaktari hawatajua kiini cha kifo chako,” aliandika Aunty Ezekiel.

image
na Radio Jambo

Habari02 August 2022 - 10:01

Muhtasari


• “Tunaishi Dunia Ambayo Rafiki zetu wanachukia Mafanikio yetu kuliko Adui zetu,” aliandika Aunty Ezekiel.

Muigizaji mkongwe wa filamu, Aunty Ezekilel

Muigizaji mkongwe kutoka Tanzania, Aunty Ezekiel amekuja na jipya, kwa kuwapa mashabiki wake mbinu rahisi ya kutaka kufa mapema, kwa wale wenye nia ya kufa lakini kifo kimewakataa.

Kulingana na muigizaji huyo, ukitaka kufa mapema basi ni rahisi kama kuhesabu takwimu moja mbili tatu, kwani unachanganya umaskini pamoja na wivu kwenye kinu kimoja halafu unaongezea ushindani, na hapo utakuwa umekikaribisha kifo kwa njia rahisi kweli kweli.

“Ukitaka kufa mapema tu Changanya umaskini na wivu basi ongeza Ushindani, niamini mimi, hata madaktari hawatajua kiini cha kifo chako,” aliandika Aunty Ezekiel.

 Mwanamama huyo ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza kwenye filamu mbali mbali na muigizaji marehemu Steven Kanumba alionekana kutupa mkwara kwa watu wa karibu naye ambaye kwa njia moja au nyingine alionekana kudokeza kabisa kwamba wanamuonea gere katika mafanikio ya maisha yake.

Katika picha nyingine aliyoipakia, Ezekiel alisema kwamba maisha ya siku hizi watu wanaishi na watu wa karibu nao ambao wanawaonea gere katika mafanikio yao.

Tunaishi Dunia Ambayo Rafiki zetu wanachukia Mafanikio yetu kuliko Adui zetu,” aliandika Aunty Ezekiel.

Mwaka 2007 alifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara maarufu Jack Pemba na kupata watoto watatu na baadaye kuoana na dansa maarufa Mosse Iyobo ambaye waliachana kabla ya muigizaji huyo mkongwe kuyaweka maisha yake ya uchumba na mapenzi faraghani mpaka sasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved