Evelyn Wanjiku Mungai, almaarufu Mungai Eve ni mmoja wa WanaYouTube waliofaulu nchini Kenya.
Yeye ndiye mpenzi wa sasa wa mpiga picha ambaye jina lake ni Director Trevor. Kuongezeka kwa haraka kwa Mungai katika YouTube ni matokeo ya usaidizi wa Trevor.
Dakika chache zilizopita Eve Mungai alipakia picha yake na mpenzi wake Trevor kwenye ukurasa wa instagram huku akimshukuru kwa yote aliyomtendea.
Eve Mungai alinukuu kwa chapisho kuwa Trevor ni mfuasi wake wa mfumo. Pia alisema kuwa anampenda hadi kifo.
"Msaidizi wangu wa mfumo @director Trevor. Naapa hamjui jinsi roho hii ya kushangaza hapa inavyonisukuma kwa bidii kuwa toleo bora zaidi la wewe. Asante sana babe kwa kuniamini! Nakupenda hadi kifo,"Mungai Aliandika.
Licha ya shinikizo kutoka kwa wanamitandao wapate mtoto, wawili hao wamezidi kuonyesha mapenzi yao kila kuchao.
HUku ungai akizungumzia hayo alidai kwamba ahataleta mtoto duniani kwa ajili ya shinikizo kutoka kwa wanamiyandao.