logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Niliishia kuoa mwanamke ambaye Siwezi kuishi bila,'Bahati asema huku akimsifu mkewe

Akitumia akaunti yake ya Instagram Bahati alishiriki picha zake na Diana Marua, pamoja na nukuu tamu.

image
na Radio Jambo

Makala22 November 2022 - 20:23

Muhtasari


  • Hata hivyo, Diana Marua amekuwa akivma mitandaoni baada ya kukiri kuwa alikuwa akilala na wazee kwa sababu ya pesa kabla ya kukutana na Bahati
Diana amshukuru Bahati kwa kuendelea kumpenda licha ya mapungufu yake

Nilitafuta mwanamke ambaye ningeweza kuishi naye, lakini niliishia kuoa mwanamke ambaye siwezi kuishi bila haya ni matamshi ya Bahati kwa mkewe.

Mwanamuziki wa Kenya Kevin Bahati amemmiminia mkewe maneno mazuri ya kutuliza moyo wake siku chache tu baada ya kujifungua mtoto wa kike.

Hata hivyo, Diana Marua amekuwa akivma mitandaoni baada ya kukiri kuwa alikuwa akilala na wazee kwa sababu ya pesa kabla ya kukutana na Bahati.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii walihisi kwamba Diana alikuwa akimuumiza mumewe Bahati kwa kufichua kwamba hata alimdanganya kwamba alikuwa anafanya biashara ya kukodisha magari ilhali alikuwa akichumbiana na wanaume tofauti.

Hata hivyo Bahati anaonekana kutotikiswa na maneno ambayo mkewe alikiri na amejitokeza kuuonyesha ulimwengu jinsi anavyompenda mkewe.

Akitumia akaunti yake ya Instagram Bahati alishiriki picha zake na Diana Marua, pamoja na nukuu tamu.

"Nilikupenda jana, nakupenda leo, na ninatazamia kukupenda zaidi kesho na kila siku baada ya hapo.... Uzuri wako, nguvu, na upendo wako hujaza furaha.

Wewe ni mwamba wangu, furaha yangu, na upendo wa maisha yangu. Nilitafuta mwanamke ambaye ningeweza kuishi naye, lakini niliishia kuoa mwanamke ambaye siwezi kuishi bila. Wewe ni Nusu Bora Yangu @Diana_Marua ❤."Aliandika Bahati.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved