logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diana Marua atimiza ndoto ya muda mrefu ya mjakazi wake, "kuona ndege kwa ukaribu"

Moja ya shauku yake ilikuwa "kuona ndege karibu zaidi" - Diana alisema.

image
na Radio Jambo

Makala05 January 2023 - 11:38

Muhtasari


β€’ Diana Marua na familia yake walisafiri kwenda Malindi kwa likizo fupi kufurahia mwanzo wa mwaka mpya.

β€’ Pamoja nao alikuwa ni mjakazi huyo na mtoto wake wa kiume.

Diana Marua wamsafirisha mjakazi wao kwa ndege kwa mara ya kwanza

Mwanablogu wa YouTube Diana Marua na mumewe Bahati Jumatano walikuwa na ziara ya kujivinjari pamoja na familia yao nzima wakiwemo watoto na mjakazi wao pia.

Marua kupitia ukurasa wake wa Instagram, alisimulia sababu ya kumpeleka mjakazi wao pamoja nao, akisema kuwa amekuwa kama mmoja wa wanafamilia wao tangu mtoto wake wa Kwanza, Heaven Bahati alipokuwa na miezi 5 tu.

Marua alisema kuwa Mjakazi huyo wao kwa jina Irene Nekesa kwa muda mrefu amekuwa mtiifu na hivi karibuni anafikisha miaka mitano kama mmoja wao katika familia hiyo yenye furaha.

“Mjakazi wangu @irenenekesa31 ni mmoja wa watu Bora ambao Mungu aliniletea. Amekuwa nasi tangu mtoto wangu @heavenbahati alipokuwa na umri wa miezi 5 na hivi karibuni atatimiza Miaka 5 katika wiki chache. Kutunzwa na Irene kwa miaka mingi kumeniletea amani na furaha nyingi sana. Nini mama yeyote angetamani kutoka kwa mlezi. Yeye ni sehemu yetu, yeye ni familia,” Marua alisema.

Pia alifichua kuwa mama huyo alianza kazi yake kama mtu wa siku lakini kutokana na utendakazi wake wa kimaadili, walimpa mkataba wa kufanya kazi kutoka boma lao ambapo walimpa ruhusa ya kujumuika na mtoto wake ambaye kipindi hicho alikuwa na miaka 4.

Marua alisema kuwa siku zote mjakazi huyo amekuwa na ndoto ya kuona ndege kwa karibu tu lakini Jumatano alimtimizia ndoto yake na hata kumsafirisha kwa ndege pamoja na mwanawe kwa mara ya kwanza katika maisha yake.

“Alikuja kama yaya wa siku na kwa sababu ya bidii yake ya kufanya kazi pande zote, nilimwajiri kama yaya wa wakati wote na kwa kuwa alikuwa na mtoto wake, Joshua ambaye alikuwa na miaka 4 wakati huo na hakuwa na mtu wa kumtunza, tulimchukua naye ndani pia. Moja ya shauku yake ilikuwa "kuona ndege karibu zaidi" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hivyo, jana, sio tu kwamba aliona ndege, bali tulisafiri naye hadi @malindidreamgarden na familia yangu pamoja na mwanawe kufurahia likizo zetu,” Marua alisema.

Watu walimshukuru kwa kuangaza nuru moyoni mwa mama huyo na pia kumtimizia ndoto yake ya muda mrefu.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved