logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pritty Vishy: Ukiamua kunitongoza basi jua utasimamia bili zote za mahitaji yangu

"Wakati unajaribu kuja kwangu kunitongoza, hakikisha unajua kwamba unakuja kusimamia bili zangu."

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 March 2023 - 09:58

Muhtasari


  • • Visjhy amekuwa bila mpenzi tangu kuachana na Stevo SImple Boy mwaka jana.
Vishy atoa ujumbe kwa wanaume.

Mwanablogu wa YouTube Pritty Vishy amefunguka kwamba tangu aanze kuongeza uzuri na urembo, wanaume wengi wamekuwa wakimtupia mistari kwenye DM za kurasa zake mitandaoni.

Mwanadada huyo kutoka mtaa duni wa Kibera sasa ameamua kutoa ujumbe wa wazi kwa wanaume hao ambao wanafurika kwenye faragha zake akisema kwamba kikubwa anachokiangalia ili kukubali mtu wa kutoka naye kimapenzi basi ni pesa.

Vishy alisema kwamba mwanamume yeyote atakayemkaribisha kwenye maisha yake ni yule atakayekuwa tayari kuchukua majukumu ya kusimamia bili zake zote ambazo kwa sasa anajigharamia mwenyewe bila mpenzi.

“Kwa wanaume wote ambao wako kila mahali wakijaribu kunitongoza, notisi ya kipoole tu ni kwamba wakati unajaribu kuja kwangu kunitongoza, hakikisha unajua kwamba unakuja kusimamia bili zangu na kufanya Zaidi ya kile ninachokifanya kwa sababu sina nia ya kurudi nyuma,” Vishy alisema.

Mrembo huyo alisisitiza kwamba anahitaji mwanamume ambaye atakuwa na uelewa wa kiwango cha juu kuhusu thamani yake na kujitoa kwa hali na mali kuigharamikia thamani hiyo.

“Nahitaji mwanamume ambaye ataelewa thamani yangu. Kwa hiyo kama uko tayari kuafikia vigezo hivyo vyote basi tunaweza chumbiana,” Vishy aliongeza.

Hivi majuzi, mwanadada huyo aliradidi maneno yake kwamba hana haja na aliyekuwa mpenzi wake Stevo Simple Boy akikanusha maneno ya baadhi ya watu kwamba anamkosa sana msanii huyo wa Freshi Barida.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved