logo

NOW ON AIR

Listen in Live

MP Salasya: Kwa nini siwezi nyoa nywele zangu

“Hii ni chapa, hakuna mtu anaweza niambia ninyoe hii nywele iko na maneno yake"

image
na Radio Jambo

Makala08 March 2023 - 06:55

Muhtasari


• Yeye aliapa kutonyoa huju akitoa sababu za uamuzi wake wa kuingia kwenye bunge na nywele za aina hiyo.

Mbunge Salasya azungumza sababu za kutonyoa nywele

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya kwa mara ya kwanza amezungumzia sababu kwa nini hawezi nyoa nywele zake.

Mbunge huyo wa mara ya kwanza ndiye mbunge wa kipekee katka bunge la 13 ambaye ana nywele ambazo zinampa taswira isiyoleta picha ya mheshimiwa moja kwa moja.

Mbunge huyo alisema kwamba hana mpango wa kunyoa nywele zake wakati wowote hivi karibuni, huku pia akizungumza jinsi waliburuzana na makarani wa bunge mara yake ya kwanza kuingia huko kuhusu nywele zake.

“Hii ni chapa, hakuna mtu anaweza niambia ninyoe hii nywele iko na maneno yake. Tulisema unanipa milioni moja kwanza ndio ninyoe lakini kwa sasa sioni sababu yoyote ya kunyoa. Huwa nailinda sana na inanifanya kuonekana wa kipekee kivyangu,” alisema.

“Kuna wakati nilipokuja huku kuna karani wa bunge mmoja aliniambia eti lazima unyoe hiyo nywele, nikasema sawa, nikasoma sheria za bunge na nikaona mbunge wa kiume ni kuvaa mavazi vizuri lakini hakuna pahali kumeandikwa kuwa lazima mtu anyoe…” aliongeza.

Mbunge huyo alifunguka sababu ya kununua gari la kifahari la Landcruiser V8 kuwa wanakijiji wake wanamuambia yeye ndiye dalili ya matumaini  na hivyo anafaa kuongoza kwa mfano mzuri.

“Wakiona nikienda na gari kubwa wanajidai kwamab huyu ni mheshimiwa wetu, ukienda na gari dogo unawapa aibu na unajua wewe kama mheshimiwa ndio kitovu cha Imani, hufai kuonesha dalili ya umasikini kwa watu wanaokutegemea,” Salasya alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved